Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha
Katibu tawala mkoa wa Arusha Drt Athumani kihamia amewataka watumishi wa Ruwasa mkoa wa Arusha kuandaa mipango kazi inayopimika ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ubora wa miradi ya maji inaendana na thamani ya fedha.
Drt kihamia ameyasema hayo Leo jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi Cha watumishi wote wa Ruwasa mkoa wa Arusha ambapo amesema kuwa watumishi wa Ruwasa wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano.
Naye meneja wa Ruwasa mkoa wa Arusha Mhandisi Joseph emanuel makaidi amesena kuwa wamekutana Kama timu ya watumishi wa Ruwasa ili kujiwekea mikakati na uelewa wa bajeti ya mwaka mpya wa fedha.
Mhandisi Makaidi amesema kuwa katika mkoa wa Arusha upatiakanaji wa maji katika maeneo ya vijijini ni asilimia 69.8 na kwamba wao Wana wajibu wa kufikisha asilimia zinazohitajika na serikali.
Aidha mhandisi Makaidi amedai kuwa kwa mwaka huu wa fedha wamepitishiwa bajeti ya Kiais Cha shilingi bilioni 10.4 ambayo itawafikisha asilimia 76.2 huku akimshukuru Raisi Samia Suluhu Hasan kwa kuwaletea bajeti ya bilioni 2.4 kwa ajili ya miradi ya kupambana na uviko.
Amedai kuwa wanategemea kuwa Hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa fedha mwezi Juni 22 watakuwa wamekamilisha sehemu kubwa ya Utekelezaji wa maji ambapo huduma ya maji itakuwa inapatikana kwa asilimia 90.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best