Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Nkasi
Watumishi wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa,wamepatiwa mafunzo ya kujikinga na moto wawapo katika mazingira mbalimbali yakiwemo ya kazi.
Huku lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kwa watumishi hao juu ya matumizi sahihi ya vyazo vya moto,kupunguza na kuzuia ajali na vifo vitokanvyo na moto.

Mafunzo hayo yameandaliwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kupitia Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Oktoba 9, 2025,
Akizungumza katika mafunzo hayo,Kaimu Ofisa Zima Moto Wilaya ya Nkasi,Staff Sajenti Cipyrian Mhuvi, amesema vyanzo vya moto katika mazingira mbalimbali kuwa ni uzembe unaosababishwa na uvutaji holela wa sigara pamoja na mapishi jikoni.
Pia hitilafu ya umeme inayosababishwa na kuzidisha mzigo kwenye vifaa vya umeme,kuunga umeme kienyeji, kutokukagua mifumo ya umeme ambapo amebainisha kuwa ni muhimu kila baada ya miaka mitatu mifumo ya umeme ikaguliwe katika majengo mbalimbali ili kupunguza na kizuia madhara yanayoweza kujitokeza.
Huku matumizi ya vifaa vya umeme kwa muda mrefu ikiwemo runinga,redio, swichi mbovu, uandaaji wa mashamba kwa kuchoma moto na uwindaji ni miongoni mwa vyanzo vya moto vinavyoweza kuleta madhara makubwa katika jamii.
Kupitia mafunzo hayo Staff Sajenti Mhuvi, alisema zipo hatua madhubuti za kuchukua ili kujikinga na moto katika mazingira mbalimbali ikiwemo mahala pa kazi, ambazo ni kutoa elimu kwa umma, kufanya ukaguzi kwenye vyombo vya usafiri na usafirshaji.
Kuzingatia matumizi sahihi ya vifaa vya umeme, kuwa na vifaa vya kuzimia moto, mapishi salama pamoja na kuzingatia ujenzi bora hasa kwa kutumia malighafi yenye uwezo wa kizuia moto kuanzia nusu saa hadi dakika arobaini na tano.


More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina