Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Mwanza
Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, wametakiwa kutenga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi na kucheza michezo mbalimbali ili kuimarisha afya zao.
Hayo yamebainishwa kati bonanza la watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela lililojumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,wavu,pete na kikapu.
Michezo mingine ni karata,drafti,kukimbiza kuku,kujaza maji kwenye chupa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michezo ya Watumishi wa Umma Kitaifa (SHIMISEMITA) yanatarajia kufanyika kitaifa mkoani Mwanza Agosti 24 Hadi Septemba 05 Septemba 2024 yakihusisha Halmashauri zote 185 nchini.
Akifungua bonanza hilo mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Egidy Teulas amesema”Tunahitaji kushinda katika mashindano haya ya SHIMISEMITA, bila uimara wa miili yetu hatutoweza,”.
Kwa upande wake Ofisa Michezo wa Halmashauri hiyo Bahati Kizito amewashukuru watumishi wote walioshiriki na kuwezesha Manispaa ya Ilemela kupata timu nzuri za michezo mbalimbali zitakazochuana katika mashindano hayo.
Rosemary Kasanga na Mecktrida Lyimo ni watendaji wa Kata za Nyasaka na Nyamh’ongolo wamesema bonanza hilo limezidi kuwaleta watumishi pamoja na kukuza mawasiliano baina yao.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania