Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amewataka watumishi wa Idara ya Ardhi wilayani humo kuimarisha mifumo yao pamoja na kuwa waaminifu na waadilifu katika kutatua changamoto za wananchi ikiwemo wa Kata ya Kiseke.
Masala ameeleza kuwa wamepata hoja zaidi ya 20 kutoka kwa wananchi wa Kata ya Kiseke kati ya hizo changamoto nyingi zilizojitokeza ni za malalamiko yanayohusiana na ardhi.
Hayo ameyabainisha Februari 29, mwaka katika kikao cha kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Kiseke ikiwa ni siku yake ya pili ya ziara ya kutembelea kila Kata kwa ajili ya shughuli hiyo, kilichofanyika mtaa wa Kabambo.
“Epuka kuingia katika jambo unalo ona kabisa hili ni la uonevu,kuna watu wanapoteza haki ,kuna watu wanaonewa,kuna watu wanatumia nguvu zao za kifedha kudhulumu watu wengine,” ameeleza Masala na kuongeza:
“Kwenye haya maeneo ya ardhi ninao ushahidi wa maeneo ya watu kuuzwa,kuna watu wamenyang’anywa viwanja,kuna watu wamejipa kazi ya udalali ya kuuza viwanja vya watu.Sisi tusishiriki kwenye hiyo dhambi,tutapata fedha kwa namna nyingine ambavyo Mungu atatubariki,”.
Sanjari na hayo Masala amemtaka Mtendaji wa Kata hiyo Masunga Mpandachalo , kuwapanga vyema watendaji wake na kusimamia maelekezo yanayotolewa na yatakayoendelea kutolewa ikiwemo la kusimamia bei elekezi ya sukari.
Aidha amewataka vongozi wa Kata na Mitaa kuwasikiliza wananchi katika maeneo yao.
Hata hivyo amesisitiza wananchi kulipa bili za maji na umeme ili huduma hizo ziendele kupatikana huku akiitaka MWAUWASA kumpatia nakala ya onyo la kumkumbusha wajibu wake mmoja wa watumishi anayelalamikiwa na wananchi wa mtaa uliopo Kata ya Kiseke.
“Lakini jambo la kupita na kutisha wananchi halikubaliki hasa kwa taasisi za umma, tuna kawaida ya kulindana mwisho wa siku tunachafua ‘image'( picha) ya serikali inaonekana imekuwa katili,haijali watu wake,”.
“Kwa sababu watu wanajibiwa ovyo na una shangaa,hawafiki katika ofisi, watendaji wetu hawa wa Halmashauri wanafanya kazi wanapotaka wao wame ‘relax’ wananchi wapo mtaani wanalalamika,wanamsema vibaya Rais wetu,”amesema Masala.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi