Na Judith Ferdinand
Watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara(RFB),wametakiwa kuwa wazalendo na kuzingatia uwajibikaji na uadilifu katika maeneo yao ya kazi,ili kuchochea maendeleo ya bodi na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu Mfuko wa Barabara Mhandisi Rashid Kalimbaga, Aprili 14,2025,mkoani Morogoro katika kikao kazi cha siku tatu kilicholenga kuleta mabadiliko katika utendaji kazi.

Huku akiwataka watumishi hao kushirikiana na Idara ili kuleta mabadiliko chanya katika maeneo ya kazi kwa ajili ya kuyafikia malengo waliyojiwekea.
Sanjari na hayo Mhandisi Kalimbaga,amesema katika kikao hicho mada mbalimbali zitatolewa ikiwemo elimu ya utunzaji wa siri za Serikali,elimu kuhusu afya ya akili pamoja na masuala ya utumishi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu na Utawala kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara, Aureus Mapunda amesema kikao hicho kitawasaidia watumishi kujikumbusha katika shughuli wanazozifanya mahala pakazi huku wakitarajia baada ya kikao hicho utendaji kazi wa mfuko huo utaboreka zaidi.

Nae Hindu Mussa ambae ni mmoja kati ya Watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, amesema,kikao hicho kitawawezesha watumishi wote kukumbukan wajibu wao kama Watumishi wa Umma lakini pia kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwemo magonjwa ya afya ya akili.


More Stories
Mbunge ataka safari za ndege kuanzia Dodoma
Mbogo aomba Tume kuchunguza madai ya waliokuwa wafanyakazi wa EAC
TMA yapongezwa kwa uboreshwaji wa taarifa za hali ya hewa