Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Jeshi la Polisi Kupitia kikosi cha kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo Nchini limewakamata watuhumiwa 1942 wa wizi wa mifugo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi decemba 2022.
Akitoa taarifa hiyo leo decemba 30.2022 kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo hapa Nchini kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA amesema jumla ya kesi 2934 zimeripotiwa katika vituo mbalimbali hapa Nchini.
ACP PASUA amebainisha kuwa jumla ya mifugo iliyokuwa imeibiwa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi hadi hivi sasa ni 14530 yenye thamani ya fedha ya kitanzania bilioni sita milioni miasaba kumi tisa elfu ishirini na nne mia sita 6,719,024,600.
Aidha ameongeza kuwa katika ufuatiliaji Jeshi hilo limefanikiwa kukamata watuhumiwa 1942 na kuokoa mifugo 4995 iliyokuwa imeibiwa hapa Nchini ambayo thamani yake ni bilioni mbili milioni mia nne arobaini moja laki moja ishirini na saba elfu na mia tano ishirini na tisa 2,441,127,529/=.
Vivile amesema Jeshi hilo limefanikiwa kuwafikisha katika mahakama watuhumiwa wa wizi wa mifugo katika mahakama mbalimbali hapa Nchini.
Mwisho kamanda Pasua ametoa wito kwa wafugaji na wakulima kufuata matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua