January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watu wawili wafariki Kipawa kwa kuangukiwa na ukuta

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online

Watu wawili wanaodaiwa kuangukiwa na ukuta wamefariki usiku wa kuamkia April 26 mwaka huu majira ya Afajiri na miili miwili ya marehemu wa familia moja.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari katika maafa hayo pia hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana imepokea majeruwi watatu wote wa kata ya Kipawa wilayani Ilala katika ajali ya kuangukiwa na ukuta.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Amana Dkt.Bryceson Kiwelu , amethibitisha kupokea vifo vya watu wawili na majeruwi mwishoni mwa wiki alfajili mara baada kukimbizwa katika hospitali ya mkoa .

“Wana familia hawa wakazi wa Kipawa wilayani Ilala mkoa Dar es Salaam walifikwa na madhara haya wakiwa usingizini baada nyumba yao kuangukiwa na ukuta wa nyumba ya jirani iliyokuwa uwanda wa juu wa eneo wanaloishi ambapo katika ajali hiyo waliofariki mama na mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka( 18)”alisema Dkt, Kiwelu.

Dkt.Kiwelu alisema katika ajali hiyo majeruwi watatu wanaendelea na matibabu afya zao zinaendelea kuimalika ambapo alisema anashukuru Jeshi la Polisi wilaya ya Ilala na majirani na viongozi wa Serikali za mitaa kwa ushirikiano wao kwa kuwawezesha kuwafikisha wahanga katika hospitali ya mkoa ya Rufaa Amana..

Kwa upande Mwingine Dkt Kiwelu aliwapongeza idara ya dharura na watumishi wa hospitali hiyo kwa kutoa huduma sahihi na kwa wakati .