December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mchungaji, Askofu, Dokta Getrude Rwakatare

Watu wasiozidi 10 kumzika Mchungaji Rwakatare

Na Mwandishi Wetu

MAZISHI ya aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God ) Mchungaji Getrude Rwakatare (70), yatafanyika Aprili 23 na hayatahudhuriwa na watu wanaozidi 10.

Akizungumza wakati akiahirisha kikao cha Bunge jijini Dodoma leo, Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema kuwa, wamepata taarifa kutoka kwa familia ikipendekeza mazishi yake yafanyike Mikocheni, jijini Dar es Salaam eneo la Kanisa la Mlima wa Moto

Spika Ndugai amesema, mazishi ya Mchungaji Rwakatare yatafanyika Alhamisi na kwamba Serikali ndiyo itakayosimamia mazishi hayo ambayo washiriki wake hawatazidi 10.

“Sisi wabunge lazima kuielewa Serikali na ushiriki wetu uwe ni kwa kadiri tunavyopewa maelekezo na Serikali,” alisema Spika Ndugai.

Mchungaji Rwakatare alifariki alfajiri juzi jijini Dar es Salaam na kwa mujibu wa mtoto wake, Muta Rwakatare, Mchungaji Rwakatare alaikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu.