November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watu 40 mbaroni kwa tuhuma wizi wa fedha za serikali kutumia mfumo bandia

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

KUFUATIA kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa jana juu ya tuhuma za wizi wa fedha za serikali kupitia mfumo wa mashine za kukusanyia mapato katika halmasahauri mbalimbali za nje ya mkoa wa Mbeya na mikoa mingine jumla ya watu 40 wamekamatwa kwa tuhuma za wizi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kaimu Mkuu wa mkoa Mbeya , Kanali Dennis Mwila amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuhusu maagizo ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yaliyotolewa jana na siku zingine za nyuma kuhusu upotevu wa mapato ambao umekuwa ukitokea katika mkoa wa mbeya na kuwa kuwa upotevu huo umekuwa ukifanyika katika mitandao ya Tehama katika halmashauri mbalimbali ndani ya mkoa wa mbeya na mikoa mingine .

“Kwanza kabisa nikiri kuwa wizi huo upo hadi sasa tumewakamata watuhumiwa 40 kutoka Jijini Dar es Salam ,Mbeya , Songwe, Ruvuma , Njombe katika wilaya za Ileje pamoja Tunduma Mji na kwamba chanzo cha wizi huo ni Dar es Salaam na mfumo huo umetengenezwa huko na timu ya wilaya ya mbarali ikishirikiana na mkoa kwa kupewa baraka na kamati ya usalama chini ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera ikaenda Jijini Dar na kukamata mtu huyo ,lakini vilevile kwa hapa mbeya na Songwe tumeweza kuwakamata waheshimiwa madiwani ,Watumishi wa halmashauri ,watalaam wa IT na wakusanya ushuru ambapo idadi yao kuwa 40”amesema Kanali Mwila.

Aidha Kanali Mwila amesema kuwa fedha zilizoibwa katika mfumo huo uliotenengezwa na wahuni hao ni shilingi million.450 ambazo zimeibwa ni Mbeya , Ruvuma , Njombe , Songwe, Rukwa hivyo niwatoe wananchi wa mkoa wa mbeya kuwa mkoa wao si shamba la bibi na watu wote waliofanya udanganyifu huo wa mapato wamekamatwa na baada ya kukamtwa siku ya tarehe 25, baadhi yao walifikishwa mahakamani na leo hii Agosti 28 , hii watafikishwa mahakamani wengine jambo hili wanaowafikisha mahakamani ni wenzetu wa TAKUKURU ,hivyo maagizo ya mh. Rais Samia yanatekelezwa yote kwa asilimia 100 na hakuna mtu ambaye atabaki salama kwa kufanya udanganyifu huu “amesema Kaimu Mkuu wa mkoa huo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali.

Akizungumzia wizi huo Naibu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mbeya ,VangSada Mkalimoto amesema kuwa mashtaka hayo yanatokana na taarifa walizopokea kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mbarali am,baye aliandika barua kuwa kuna ubadhilifu wa fedha wa mfumo kukusanya fedha za serikali katika halmashauri na kushauri ufanyike uchunguzi na kuomba ufanyike uchunguzi na kutokana na untyeti wa suala hilo waliwasiliana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya na kutoa maelekezo kuwa Mkuu wa wilaya ya mbarali aunde tume maalum ya kufanya uchunguzi wa suala hilo na kuundwa tum,we iliyoshirikisha , Takukuru ,polisi , usalama wa taifa na walipofanya ufatiliaji kwa utekelezaji kwa viongozi waliokuwa wameutoa katika kipindi hicho ikiwemo maelekezo ya Rais Samia ya kipindi hicho na jana.

Aidha amesema kuwa katika wizi huo walibaini kuwa wizi wa aina mbili ambao ni uhujumu uchumi wa kuisabishia hasara serikali ,wakusanya ushuru katika halmashauri mbali mbali ambao walikuwa wakitumia simu zao za mkononi ambazo zilikuwa zimeunganishwa na printer wakiwa na mashine za kukusanya usghuru za serikali wanaacha kutumia mashine za serikali wanatumia za simu zao na kutumia simu zao ambazo zinatoa nembo za halmashauri zao.

Hata hivyo amesema kuwa leo wameweza kuwafijkisha mahakamani tena watuhumiwa 14 ambao walitengeneza Tovuti ambayo ilikuwa imeunganishwa na mashine mbali mbali za kukusanya mapato na mmiliki wa tovuti hiyo ni mwananchi wa kawaida tu ambaye aliwaajiri wataalam wa Tehama wa halmashauri wakishikirikiana na mtengeneza mfumo bandia Jijini Dar es Salaam Robert Mpeleta mmiliki wa mfumo bandia na kuanza kusghirikiana watengeneza ushuru wa halmashauri mbali mbali ambao wanawapa mashine hizo kila wakikata ushuru inasoma ushuru kwenye mfumo wake .

Aidha amesema kuwa toka Januari 2022 ,wameweza kubaini kuwa mfumo huo feki wameweza kukusanya fedha nyingi na zingine zinaendelea kutafutwa na mpaka sasa hivi wameweza kukamata watu 14, ambao wameonekana kukusanya fedha sh.mil.382 katika kipinsdi hicho zimeweza kuingia kwenye mifuko yao kwa kutumia mfumo huo ndo sababu wamekatwa wote, miongoni mwa makiosa ambayo wanashtakiwa nayo ni makosa ya kimtandao kumiliki kifaa cha cha mtandao kutumia kwa njia haramu , kutengeneza genge la kiuhalifu , makosa ya utakatishaji fedha kwasababu wameweza kufatilia mali wanazomiliki na zingine tayari wamezibaini na utaratibu wa kuzishikiria unaendelea .