Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Abiria 19 waliokuwa kwenye ndege ya Precision Air iliyotumbukia Ziwa Victoria ilipokuwa ikikaribia uwanja wa ndege Mkoani Kagera wamefariki dunia.
Hayo ameyasema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofika Mkoani humo leo Novemba 6, 2022
Kufuatia kuongeza kwa watu waili kutoka 43 na kuwa 45 katika ajali hiyo, Waziri Mkuu ameagiza uchunguzi kufanyika ili kufahamu watu hao wawili ni akina nani na wametoka wapi.
”Uchunguzi ufanyike ili kujua hao wawili wanaoongezeka kwenye idadi wametoka wapi, kama ni miongoni mwa walioenda kuokoa au kama ni watumishi wa ndege hawakuandikishwa” – Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa, kwa namna ndege hiyo ilivyotumbukia katika ziwa Victoria kwa kutanguliza kichwa hakuna matumaini ya rubani wa ndege hiyo kuwa hai.
Lakini pia Waziri Mkuu amesema uchunguzi wa chanzo Cha ajali unaendelea na vyombo husika ili kupata taarifa sahihi za kilichotokea kwa sababu ndege ilivyoanguka kichwa kinaonyesha ndege ilikuwa inaondoka wakati ilikuwa inatua.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua