Na Heri Shaban, Timesmajira Online,Ilala
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema wilaya hiyo inatarajia kutoa chanjo aina mbili kwa watoto zaidi ya 2000 wenye umri chini ya miaka mitano.
Akizungumza katika kikao cha uraghibishaji wa hamasa ya huduma za chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema jumla ya watoto 2550 wanatarajia kupatiwa chanjo aina mbili ambazo ni Penta na MR2 kwani Halmashauri hiyo haijafikia lengo la asilimia 100 katika utoaji wa chanjo hiyo.
“Tunatarajia kutoa chanjo ya Penta na MR2 kwa watoto chini ya miaka mitano ambapo katika awamu hii Halmashauri ya Jiji itafikia asilimia 100 kutokana na kujipanga kikamilifu,”amesema Mpogolo.
Mpogolo amesema watoto 1653 hawakumaliza chanjo zao wilayani Ilala ambapo makundi hayo mawili watapata huduma hiyo katika mfumo huo wa uraghibishaji chanjo.
Amesema dhumuni la chanjo hizo ifikie watoto 1033 katika chanjo ya Penta walifikia watoto 1029 sawa na asilimia 96 na kwa upande wa MR2 walifikia watoto 1029 kati ya watoto 1033 sawa na asilimia 90 4 .
Katika hatua nyingine alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Zaituni Hamza kwa utendaji bora wa kazi pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEIF )kupitia taasisi ya Tanzania Interfaith Partineship (TIP)na chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Radhid Mfaume amepongeza maandalizi ya mkakati huo kabambe wa uraghibishaji chanjo na kwamba utaleta ufanisi katika kuwafikia watoto hao waliokosa au kukatisha chanjo.
Mganga Mkuu kuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Zaituni Hamza, ameeleza kuwa chanjo hiyo itatekelezwa katika maeneo yote ya jiji hilo hasa yale yalio katika tishio kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wakati kampeni hiyo ikitekelezwa katika vituo vya afya .
Ofisa wa Program sehemu ya Elimu kwa Umma Wizara ya Afya Simon Zilimbili amesema chanjo hiyo itafanyika kwa siku kumi katika tarafa tatu wilayani Ilala lakini zaidi katika tarafa mbili ambazo ni Ukonga na Segerea ambazo zimeonekana kuwa na changamoto.
“Tunaelekeza chanjo hii katika maeneo yenye tushio la mlipuko kutokana na mvua inayoendelea kunyesha ,makazi mapya na yalio na watoto wengi,”amesema Zilimbili.
Amesema katika Tarafa ya Ukonga na segerea kata 26 zitafikiwa na kaya 259,200 kati ya kaya 458 ,614 zitafikiwa.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi