Suleiman Abeid,Timesmajira Online, Shinyanga.
JAMII mkoani Shinyanga imekumbushwa wajibu wa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum kwa kuwapatia misaada mbalimbali itakayo wawezesha kuishi kama watoto wenzao waishio na wazazi ama walezi wao.
Ombi hilo limetolewa na Diwani wa Kata ya Mjini Shinyanga, Gulam Hafidh Mukadamu wakati akikabidhi msaada wa vyakula kwa watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma kwenye shule ya msingi Buhangija Jumuishi iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Gulam amesema watoto wanaolelewa na kusoma katika shule ya msingi Buhangija Jumuishi wanahitaji kupatiwa misaada ya mara kwa mara ili waweze kuishi vizuri na kusoma kwa ufanisi.
Ambapo jamii haipaswi kuiachia Serikali pekee yake mzigo wa kuwalea watoto hao,hivyo yeye na familia yake leo wamesukumwa,wakaona wafike katika shule hiyo kuwatembelea watoto hao wenye mahitaji maalum wakiwemo wasioona, wenye ualbino na wenye usikivu hafifu (viziwi).
Lengo likiwa nikuwapatia msaada kidogo utakaoweza kuwasaidia katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
Diwani Gulam Hafeez Mukadam akimtambulisha mkewe mbele ya watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma shule ya msingi Buhangija Jumuishi Shinyanga.
“Jamii inapaswa kuelewa kuwa watoto hawa pia wana haki ya kuishi kama wanavyoishi watoto wenzao wenye wazazi wawili ama walezi wao, hivyo tuhakikishe kila baada ya muda tunawatembelea na kuwaletea misaada mbalimbali ikiwemo vyakula, nguo na mahitaji mengine muhimu,” ameeleza Gulam.
Amesema yeye na familia yake wameweza kutoa mchele kilo 50, unga wa sembe kilo 30,sukari kilo 25, chumvi kilo 5, sabuni ya unga kilo 25, sabuni ya vipande boksi 1, nyama kilo 10, viazi mviringo kilo 10 pamoja na tambi katoni 1 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 700,000.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi shule ya msingi Buhangija Jumuishi, Rose Daudi ametoa shukrani zake kwa familia ya Diwani huyobkwa jinsi ambavyo amekuwa akiwakumbuka mara kwa mara watoto hao hasa ikizingatiwa yeye ni miongoni mwa waanzilishi wa kituo hicho.
Ambapo ameeleza kuwa msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza baadhi ya mahitaji walionayo katika shule hiyo.
“Shule yetu ina jumla ya watoto 201 ambao wamegawanyika katika makundi matatu wakiwemo wenye ualbino, wasioona na wale wenye usikivuu hafifu vizuri (viziwi), hivyo utaona jinsi gani pana kila sababu ya kupatiwa misaada kila mara ili kupunguza changamoto ya uhaba wa mahitaji hasa upande wa chakula,” ameeleza Rose.
Kwa niaba ya wanafunzi wenzao,John Daima na Neema Malimi wameishukuru familia ya Diwani huyo kwa msaada walioutoa kwao ambapo wamemuomba Mwenyezi Mungu awarejeshee katika sehemu ambayo wameitoa na kwamba wamefarijika sana kuona na wao wakikumbukwa.
Diwani Gulam Hafidhi Mukadam (mwenye miwani) akikabidhi msaada wa vyakula kwa watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma shule ya Msingi Buhangija Jumuishi Manispaa Shinyanga.
Mtoto Neema Malimi akitoa shukrani kwa familia ya diwani Gulam baada ya kupokea msaada.
Mwalimu Mkuu Msaidizi shule ya msingi Buhangija Jumuishi Manispaa ya Shinyanga, Rose Daud akitoa shukrani baada ya kupokea msaada.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi