November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watoto Wawili wauwawa na mama yao kwa kukatwa na Panga

Na Esther Macha, TimesMajira, Online ,Mbeya

WATOTO wawili wa familia moja wakazi wa mtaa wa Ilolo Kata ya Sinde mkoani Mbeya wameuwawa kwa kukatwa na Panga kichwani na mikononi na mmoja kujeruhiwa na Mama yao mzazi aitwaye Shari Mwambamba (27).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amemtaja mama mzazi aliyefanya mauaji ya watoto kuwa ni Shari Mwambamba (27).

Aidha Kamanda Kuzaga aliwataja watoto waliouwawa kuwa ni Neema Chembe (07)Leonard Chembe mwaka mmoja na nusu na ambao wote walikutwa wameuwawa kwa kukatwa na Panga sehem za kichwani na mikononi na mama yao. Hata hivyo amesema mama huyo aliendelea na mauaji kwa kumjeruhi mtoto wake mwingine aitwaye Emmanuel Chembe (03) pamoja na mdogo wake aitwaye Nuru Mwambamba (23)wote wakazi wa mtaa wa Ilolo Kata ya Sinde ambao wote wamepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa matibabu.

Kamanda Kuzaga amesema chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa ingawa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa November 20 majira ya saa 4.30 usiku Mtuhumiwa akiwa nyumbani na mume wake aitwaye Evarist Chembe (45)mlinzi wa kampuni ya Anazindua Group alianza kuweweseka na kuongea vitu visivyoeleweka akimkumbuka mdogo wake aliyefariki dunia kwa kujinyonga huko Usangu wilaya ya Mbarali.

Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu na mtuhumiwa amepelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya idara ya magonjwa ya akili kwa uchunguzi wa kitabibu.

Akingumza na waandishi wa habari akiwa eneo la tukio Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Ilolo Ngambi Kulaba alisema kuwa tukio hilo ni la kusikitisa ambalo Halijawahi Kutokea Katika katika mtaa huo na kusema kuwa alifuatwa nyumban kwake na mwenye nyumba kuwa waende nyumbani kwake kuwa kuna mauaji ndipo alipochukua jukumu la kupiga simu Polisi haraka na kufika eneo la tukio.

Kulaba amesema l kuwa kuchungulia dirisha waliona mwanamke amelala kifudifudi ndipo wakafungua mlango na kugundua kuwa ni Mama mzazi wa watoto hao ndiye aliyehusika na mauaji hayo.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa mtoto mmoja alinusurika kuchinjwa na mamaake huyo baada ya kujificha chini ya uvungu wa kitanda ambako mama huyo alikuwa akitekeleza mauaji hayo hivyo uongozi wa mtaa tunawakabidhi Polisi kwa hatua zaidi.

Hata hivyo amesema kuwa kitendo hicho ni kibaya na kila niwe katika mtaa huo na kwamba tukio hilo litazidi kuchunguza.

Kwa upande wake ASP Nimbwelu Mwalukasa Ni Mkuu Wa Ushirikishwaji wa Jamiii wilaya ya Mbeya Mjini na Kaimu Mkuu wa upelelezi wilaya amesema kuwa tukio hilo ni kubwa hivyo wananchi wawe watulivu kwani mpaka Sasa hawajampata mtuhumiwa wa mauaji ni nani yapo jamii Inamuhusisha Mama Mzazi.