November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watoto wakamatwa wakisafirishwa Ulaya

TRIPOLI, Zaidi ya watoto 100 waliokuwa wanasafirishwa kwenda Ulaya ni kati ya wale waliokamatwa baharini na mamlaka ya Libya nje ya Pwani ya bahari ya Mediterranean.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Watoto (UNICEF) watoto 125 wamekamatwa na wengi wanashikiliwa katika vituo mbalimbali.

UNICEF imefafanua kuwa, watoto ambao wanakimbia vita na umaskini hutumia usafiri hatari wa baharini kuelekea Ulaya na ulijumuisha watoto 114 waliosafiri peke yao.

“Wengi wa wale waliookolewa wanapelekwa katika vituo vya kuwashikilia ambavyo vina msongamano nchini Libya vyenye hali mbaya kabisa na bila au kiasi kidogo cha upatikanaji wa maji na huduma za afya. Takribani watoto 1,100 wako katika vituo hivi,”imeeleza taarifa hiyo.

UNICEF imezisihi mamlaka nchini Libya kuwaachia watoto wote na kuacha kuwashikilia katika vituo vya uhamiaji nchini humo.