Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali wametakiwa kutumia maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa sabasaba kupita katika Banda la FCC kupata elimu itakayowasaidia kuepukana na kujishughulisha na bidhaa bandia na vitendo vingine ambavyo haviruhusiwi na Sheria ya ushindani
Rai hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa FCC, William Erio wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema zoezi hilo likifanyika litawasaidia watoa huduma hao wafanye biashara halali na serikali nayo inufaike kwa kupata kodi.
“Tumeshaanza kutoa elimu na tutakua tunatoa elimu hiyo katika kipindi chote Cha maonesho”
Pia Erio ametumia maonesho hayo kuwakumbusha watanzania vigezo ambavyo vinafanya Tanzania kuwa ni mahala sahihi kufanya biashara na uwekezaji.
“Kwanza ni sera nzuri za uwekezaji zilizo wekwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.”
“Lakini kuna vigezo vyote ni muhimu ambavyo uwekezaji unafanyika upatikanaji wa mali ghafi katika nchini kuna miundombinu kuwezesha wawekezaji kama vile upatikanaji wa umeme na njia za usafirishaji.”
“Upatikanaji nguvu kazi katika sensa iliyofanyika. Mwaka juzi Tanzania ina watanzania zaidi ya milioni 60 hivyo muwekezaji yeyote ana uhakika wa nguvu kazi.” Amesema Erio
Mbali na hayo, Erio amesema jambo jingine muhimu ambalo linavutia uwekezaji na lina rahisisha kufanya biashara ni kuwa na Taasisi za usimamizi wa shughuli za kibiashara ambazo zipo imara ambazo pia zitahakikisha ufanyaji wa biashara hakuna mtu anafanya biashara kwa kutumia mbinu adaifu na chafu za kuwakwamisha wengine kwa lengo la kuwatoa sokoni.
“Hakuna atakae fanya biashara kwa kutumia bidhaa bandia jambo ambalo litaathiri kwa wale wanafanya biashara halali na wanaozalisha bidhaa ambazo ni sahihi.”
“Yote hayo yanaweza yakafanikiwa kama FCC watafanyakazi yao vizuri pamoja na kuchukua hatua za kusimamia hayo moja wapo ya majukumu wanayofanya ni kutoa elimu ili waelewe madhara ya kufanya biashara ambazo zinadhoofisha wengine wasifanye biashara kwa soko hilo hakuna sababu ya kufanya idadi ya watu kwa soko walilonalo.” Amesema
Kadhalika, Erio amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji kutokana na kuwepo kwa sera nzuri ikiwemo kuwepo kwa Mamlaka inayodhibiti bidhaa bandia kama vile FCC
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu