Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema kitawatambua kwa majina watendaji wote wa serikali wadhembe, wababaishaji na wanaowanyanyasa wananchi ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Hayo yamesemwa leo na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda wakati alipopokelewa na wananchi wa Kijiji cha Hedaru Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Aidha Makonda amesema Kwa wale viongozi wanaofanya vizuri iwe kwenye ardhi, maji au umeme tutawatambua na kuwashukuru kwa mchango na wema wao kwa Taifa letu
“Upande mmoja wapo wanaofanya vizuri lazima watambulike na waheshimike, upande wa pili wapo wanaofanya vibaya lazima wachukuliwe hatua ili mwisho Chama ishike hatamu”
Kuhusu changamoto wanazokumbana nazo wananchi hao, Makonda amesema atawatafuta mawaziri husika ili watoe majibu ya hatua wanazochukua kuhakikisha kwamba wananchi hao wa same na Kilimanjaro kwa ujumla wanakua na uhakika na usalama wa maisha yao hasa wale wanaouwawa na Tembo.
“Yapo mambo hapa ikiwemo umeme, ni ukweli usiopingika, changamoto ya umeme ipo, kuna maji ni ukweli usiopingika changamoto hiyo ipo, kuna barabara, TARURA wanajipanga kwaajilili ya kuhakikisha wanarekebisha lakini ipo pia migogoro ya ardhi na mipaka, pia wanayama wanaowatesa na kuwaumiza wananchi wa Wilaya ya same, nikifika same nitapata majibu kama siyo kwangu tutawatafuta mawaziri husika watuambie hatua wanazochukua kuhakikisha kwamba nyinyi wananchi wa same na wanakilimanjaro kwa ujumla mnakua na uhakika na usalama wa maisha yenu hasa wale wanaouwawa na Tembo” Amesema Makonda
Matukio mbalimbali katika picha
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa