Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kampeni ya kuhamasisha matumizi ya NMB mastercard na QR Code ‘Lipa Mkononi’ iitwayo NMB MastaBata ‘Kote Kote’, imefikia ukomo kwa wateja 7 na wenza wao kujishindia safari ya Dubai kwa siku nne inayogharamiwa kila kitu na Benki ya NMB.
Kampeni hii imeendeshwa kwa miezi mitatu na kutoa zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 350 kwa washindi.
Akizungumza katika droo hiyo ya fainali Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB – Filbert Mponzi aliwataja washindi hao kua ni: Upendo Yohana Msanjila (Dar), Edwin Sett Mwakabage (Kilimanjaro), Benigna Xaveria Hyera (Dar), Nazia Abdulsatar Lakha (Dar), John Wayne Lubisha (Dodoma), Chintan Chandrakant Kamania (Dar) na Qamara Rose Aloyce (Arusha).
Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ msimu wa nne ilizinduliwa Oktoba 28 mwaka jana ili kuchagiza matumizi yasiyohusisha pesa taslimu ‘cashless’ Kabla ya ‘grand finale’ hiyo, jumla ya washindi 750 walishinda pesa kiasi cha Sh.100,000 kila mmoja, wengine 98 wakizawadiwa Sh. Mil. 1 kila mmoja, huku washindi 12 wakitwaa bodaboda moja moja zenye thamani ya Sh. Mil. 3 kwa kila moja na washindi wengine wanne wakijishindia safari ya Zanzibar kuhudhuria Tamasha la NMB Full Moon Party.
Kampeni hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa kwa kufanikiwa kubadili tamaduni za matumizi ya kadi na QR Code ambayo ni salama, rahisi na nafuu zaidi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa