January 18, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watatu wafariki, ajali ya ndege Bukoba

Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, Bukoba

Jumla ya abiria 26 wameokolewa wakiwa hai Kati ya 43 na miili 3 ya marehemu waliokuwa kwenye ndege ya Precisison Air yenye usajili namba ATR 42,5HPWF iliyoanguka kwenye ziwa Victoria Mita ,( 100 ) kabla ya kutua uwanja wa ndege Bukoba.

Taarifa hiyo imetolewa na Mganga mkuu wa Mkoa wa Kagera,Dk. Issesanda Kaniki wakati akiongea na waandishi wa habari eneo la tukio.Dk.Kaniki amesema Kati ya majeruhi 26 wanaume ni 17,wanawake 9 na katika vifo vitatu wanawake wanaume ni wawili na mwanamke mmoja .

Amesema majeruhi wanaendelea kupatiwa huduma katika hospital ya rufaa ya mkoa na uokoaji bado unaendelea.Mkuu wa mkoa wa Kagera ,Albert Chalamila, amesema Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Jijini Dar -es- Salam kupitia Mwanza kuja Bukoba Mkoani Kagera.Chalamila,anasema licha ya changamoto ya Ndege hiyo kuanguka katika ziwa Victoria bado Kuna mawasiliano na marubani wa ndege hiyo.

Amesema jitihada za uokozi wa Ndege na abiria na mizigo yao zinaendelea kwa kutumia vifaa vya kusasa ambavyo wameagiza kutoka Mkoani Mwanza,Geita na kiwanda Cha Kagera sugar.

Amesema wananchi wametoa ushirikiano wa kutosha katika maokozi hayo na kuwataka kuendelea kuwa watulivu.

Hata hivyo amesema waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania atawasili katika viwanja hivyo kushiriki zoezi la maokozi.