March 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania wahimizwa kulinda,kuenzi utamaduni 

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza 

Wito umetolewa kwa Watanzania, kuhakikisha wanalinda,kuuenzi,kudumisha na kuupigania utamaduni wa kitanzania,ili  kuchochea maendeleo ya taifa na maadilia katika vizazi vya sasa na vijavyo.

Hayo yamezungumzwa  Machi 8,2025,na Mkurugenzi wa Cheza Kidansi Entertainment na Mratibu wa tamasha la Chifu Hangaya Utamaduni 2025(Chief Hangaya Utamaduni Festival 2025), Bernard James,wakati wa tamasha hilo kilifanyika uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela mkoani Mwanza,ambalo likitumika kusherekea siku ya Wanawake Duniani.

“Taifa lolote ambalo halina  utamaduni,ni sawa na taifa mfu,kila mtu anawajibika rasmi kuenzi,kuupugania na kutetea utamaduni wetu wa kitanzania ambao ni mzuri na unachochea watalii kuja kufanya utalii ikiwemo kujifunza lugha yetu ya Kiswahili.Ambapo utalii uanachangia kwa asilimia kubwa katika pato la Taifa,” amesema Bernard.

Bernard amesema,tamasha hilo  la Chifu Hangaya Utamaduni lilianza mwaka 2023 na utekelezaji wake rasmi umeanza mwaka 2025,ambalo lengo lake ni kuenzi utamaduni wa kitanzania.Ambapo katika tamasha hilo limetoa fursa ya makabila zaidi ya 100 yaliopo nchini hapa kushiriki na kuenzi tamaduni zao.ikiwemo Wahaya, Wasukuma na Wajita.

“Tumetumia tamasha hili kuwapongeza wanawake nchini katika siku yao akiwemo Rais Samia  Suluhu Hassan ambaye ukimyizama unaona kalelewa katika maadili,malezi mazuri ya utamaduni wa kitanzania,hivyo bila wanawake  hatuwezi kuenzi  utamaduni,” amesema Bernard.

Ofisa Utamaduni na Michezo Mkoa wa Mwanza James William, amesema, utamaduni ni maisha kwa ujumla  na kitambulisho cha kila mtu na taifa ikiwemo mavazi,ambayo imekuwa ikienezwa kwa njia ya sanaa mbalimbali kama nyimbo,sarakasi na ngoja.

“Na taifa lisilo na utamaduni,ni kama taifa lisilo kufa,sisi Watanzania tumeruthi utamaduni mzuri toka kwa mababu zetu ikiwemo Mila, desturi,mavazi na lugha nzuri ingawa kwa sasa kutokana na utandawazi  tumeanza kupuuza lugha zetu,mfano ukiongea kisukuma  wakati mwingine unaonekana ujasoma lakini ukiongea kiingereza  unaonekana msingi.Hii siyo nzuri inaharibu mila,desturi za lugha zetu,”amesema James.

Pia amesema, utamaduni wa Mtanzania nimkufanya kazi,hivyo wauimarishe utamaduni huo kwa kufanya kazi kwa bidii.

“Serikali inathamini utamaduni wa Watanzania na itaendelea kutoa mchango wake kwa kadri na wakati ili uendelee kuenziwa na kudumu,”.

Kwa upande wake Chifu Musiba himaya ya Buchosa Geita,ambaye ni mwanamke,amewahimiza wanawake popote walipo kuenzi utamaduni wao pamoja na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu.

 Kuhani Mkuu wa  Rastafari King Valerian Bagaile, amesema,wamekutana katika tamasha hilo ambalo limetoa elimu na kurudisha maadili na utamaduni  wa kitanzania.