Na George Mwigulu, TimesMajira, Online Mlele.
WANANCHI hasa jamii ya wafungaji Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuwathamini wanyama wanaowafuga kwa kuwapatia huduma za kitabibu kwa mabwana mifungo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Wito huo umetolewa na mratibu wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko wa Hosptali Teuli ya Rufaa mkoani Katavi Dkt. Taphinez Machibya, wakati akitoa elimu kwa wafugaji namna ya kuepuka ugonjwa wa homa ya bonde la ufa kwa kuhakikisha chanjo kwa mifugo inatolewa kila mara.
Dkt. Machibya amesema homa ya bonde la ufa husababishwa na virusi vinavyosababisha athari kwa wanyama wa kufungwa ikiwemo ng’ombe, mbuzi, kondoo na ngamia.
“Wanyama wanapokuwa wameathirika na wakati huo wanyama hao wakatumiwa na wanadamu kama kitoweo au kugusa majimaji yaliyotoka puani, damu na mkojo ndio itakuwa njia kuu ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa mlipuko wa homa ya bonde la ufa,” amesema.
Daktari huyo alifafanua kuwa wanyama ambao wako tayari wamepata maabukizi ya ugonjwa huo ni vigumu kuwatambua haraka kwa kuwatazama kwa macho, bali inafaa kila wakati kuwaita wataalamu wa mifungo kuja kufanya uchuguzi wa kitabibu.
Amekemea baadhi ya tabia ya wafugaji wenye mila na desturi za kuchinja wanyama wagonjwa kwa dhana potofu ya kuwawahi kabla ya kujifia ili wapate kitoweo, kwani vitendo hivyo ni hatari kwa walaji na wanakuwa na uwezekano wa kupata ugonjwa wa homa ya bonde la ufa na magonjwa yanayosababishwa na ulaji wa nyama.
Vile vile aliwaambia wafugaji hao kuwa dalili ya homa ya bonde la ufa kwa binadamu ni kupata maumivu ya kichwa, kutapika, kuhalisha na pamoja na maumivu ya tumboni kwa sababu virusi hivyo huathiri mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
Aidha, Dkt. Machibya amewashauri wafugaji na jamii kwa ujumla kuwa pindi waonapo dalili hizo ni muhimu kufika hosptalini kwa ajili ya matibabu ambako yanapatikana.
Mmoja wa wafungaji wa Kijiji cha Masingo Wilaya ya Mlele, Ng’andu Jimisha alimshukuru Dkt. Machibya kwa elimu aliyowapatia, kwani itawasaidia kujilinda na ugonjwa huo hatari.
Jimisha amesema kuwa kama afya za mifugo itakuwa haina magonjwa, vile vile afya za watumiaji zitakuwa salama zaidi. Naye, Sayi Luhende mfugaji wa Kijiji cha Mapili wilayani humo, alisema licha ya ugonjwa wa homa ya bonde la ufa kutosikika sana, lakini hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali za kuwaelimisha wananchi zitasaidia kuutokomeza zaidi.
Luhende ameiomba Serikali kuongeza juhudi zaidi ili kutokomeza ugonjwa huo kwa kuhakikisha upatikanani kwa urahisi wa chanjo za mifungo.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati