November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watakiwa kushirikiana kutikomeza matatizo ya lishe

Na Ashura Jumapili TimesMajira Online, Kagera

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Siima,amewasisitiza watendaji wa afya,elimu, maendeleo ya jamii,kata na wananchi, kushirikiana kutokomeza matatizo ya lishe kama udumavu,ukondefu na utapiamlo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha lishe,ilieleza kuwa hali ya lishe kipindi cha Julai hadi Septemba 2024 imeimarika kwani watoto wenye utapiamlo mkali ni asilimia 0.1,watoto wenye udumavu asilimia 0.2 na watoto wenye ukondefu ni asilimia 0.6.

Hayo yamefanyika katika kikao cha tathmini ya lishe ngazi ya Wilaya cha robo ya kwanza 2024/25 kilichofanyika Novemba 15,2024 katika ukumbi wa makao makuu ya Halmashauri hiyo.

Ambapo Kata zilifanya vizuri katika utekelezaji wa afua za lishe kwa robo hiyo, ikiwemo Kata ya Ruhunga, Nyakibimbili, Nyakato,Kishanje na Katoro.Huku Watendaji wa Kata hizo wakipatiwa zawadi na Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukoba Fatina Laay, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao.

Sanjari na hayo Waganga Wafawidhi kutoka vituo tisa vya afya kikiwemo cha Katema,Bujugo,Nyakibimbili,Butulage,Buzi,Ruhunga,Kishogo,Kaagya na Nsheshe,walikabidhiwa vibao vya kupimia urefu watoto chini ya umri wa miaka mitano.