Na Queen Lema, Timesmajira Online,Arusha
Wanawake wajasirimiali waliopo sokoni nchini hapa wametakiwa kuwa katika vikundi vya umoja ili waweze kufikiwa na fursa mbalimbali kama vile za kiuchumi pamoja na za kiteknolojia ambazo wakati mwingine hutolewa kupitia vikundi
Hayo yameelezwa na Jane Mgigita kutoka Asasi ya Equality for Growth wakati akiongea na wajasiriamali wanawake kutoka katika soko la Kilombero ambao walitembelewa na wadau kutoka katika katika mkutano wa Asasi za kiraia(Azaki) unaendelea Arusha.
Jane amesema kuwa mwanamke wa sokoni mara nyingi huwa anaamka kwake yeye kama yeye na kwa kuwa anajitafutia mwenyewe lakini ili aweze kufikiwa na fursa mbalimbali anatakiwa kuwa na wengine.
“Nawasihi wakina mama wa sokoni hakikisheni kuwa mnakuwa wamoja hasa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi huwezi kupata huduma iwapo upo pekee yako lakini mkiwa wengi ni rahisi sana kuweza kusaidia kama kikundi,”amesema.
Wakati huo huo aliishauri Serikali kuhakikisha kuwa wanaendelea kuboresha mifumo ya wanawake sokoni ili kuweza kuwasaidia kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
“sisi kwa kutambua hilo tuna mradi ambao tumeshautekeleza kwenye baadhi ya mikoa ila Arusha nayo ipo mbioni,tunataka kuona wanawake wa sokoni nao wanapata haki zao za msingi hasa kwa kuwaboreshea mazingira,”.
Naye Wakili kutoka katika Shirika la Legal Service Facility Deo Bwire amesema kuwa wanawake wa sokoni wanaitaji mara kwa mara kuwa na mikutano na wanasheria ambapo sasa watalamu wa sheria wataweza kuwasaidia hasa kwenye masuala yanayohusiana na haki zao za msingi.
Wakili Bwire amedai kuwa wakati mwingine wajasiriamali hasa wanawake wanashindwa kupata haki zao kwa kuwa hawajui kuitafsiri sheria hasa kwa lugha ya Kiswahili.
Naye Diwani Kata ya Levolosi Agustino Matemu amesema kuwa kwa sasa wanawake hawapaswi kukaa nyuma bali wanatakiwa waweze kunyanyuka tena kwa kumuangalia Raisi Samia Suluhu Hassan.
Matemu amesema kuwa atahakikisha anapaza sauti za wanawake hasa pale wanapoonewa au kukandamizwa na sheria kwani kwa sasa kundi hilo linachangi sana ongezeko la uchumi.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi