Na Mwandishi Wetu,Dar
BAADHI ya wasusi jijini Dar-es-Salaam wameiomba kampuni ya Darling Hair kupanua wigo wa programu yake ya Loyalty Program ili kuwafikia wasusi wengi zaidi, wakisema mpango huo umekuwa na manufaa kwao katika kipindi cha miaka miwili tangu kuanzishwa kwake.
Rai hiyo imetolewa katika hafla ya kutimiza miaka miwili ya programu hiyo iliyowakutanisha wasusi kutoka Kariakoo,Magomeni,Manzese na maeneo ya jirani katika ukumbi wa Sinza Deluxe, jijini Dar-es Salaam. Hafla hiyo ilihusisha michezo, muziki, vyakula, zawadi na burudani mbalimbali.

Queen Mgao,msusi kutoka Kariakoo amesema,kuongezwa kwa idadi ya wasusi wanaonufaika na programu hiyo kutawapa fursa zaidi ya kukusanya lebo na pointi zinazowawezesha kupata vifaa mbalimbali vya saluni.
Kwa mujibu wa Mgao, programu hiyo imewasaidia baadhi ya wasusi kupata vifaa vya saluni bila kulazimika kutumia fedha zao kununua vifaa hivyo Ambapo amesema wasusi ukusanya lebo kwa malengo na wanapofikisha kiwango kinachohitajika, wanaweza kuchagua kifaa wanachostahili kupata kama zawadi.
Johari Iddi msusi kutoka Kariakoo amesema,maadhimisho hayo yamekuwa fursa ya kuwakutanisha wasusi na kubadilishana uzoefu,hivyo alitoa wito kwa wasusi ambao bado hawajaingia kwenye programu hiyo kujiunga.
Msusi mwingine Evarista Henry amesema programu hiyo imewapa wasusi fursa ya mafunzo na maarifa yanayohusiana na shughuli zao pamoja na kunufaika na zawadi,huku ufuatiliaji unaofanywa na kampuni hiyo umekuwa ukisaidia katika kushughulikia changamoto zinazowakabili wasusi.
Nelson Muhigi, ambaye alianza shughuli zake Kariakoo na kwa sasa anafanya kazi Zanzibar amesema,bado anaendelea kunufaika na programu hiyo licha ya kuhama eneo la kazi ambapo mpaka sasa wameisha faidika kwa miaka miwili.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakilishi wa Darling Hair kutoka Idara ya Masoko, Daniel Kisusange amesema programu hiyo inalenga kuongeza idadi ya wasusi.


More Stories
TCRA,Wadau Rukwa wakutana kujadili uhalifu mtandaoni
Hospitali Kaliua yapokea vifaa vya kujifungulia
Malisa aagiza watumishi kutatua kero za wananchi