November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wasomi watetea mikopo kwa nchi

*Wasema miradi mikubwa haiwezi kujengwa kwa makusanyo ya mapato ya ndani, wapongeza Serikali kwa kukopesheka

Na Mwandishi Wetu

WASOMO wa kada mbalimbali nchini wameunga mkono Serikali kuendelea kukopa fedha kwa ajili ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo, kwani maendeleo hayawezi kupatikana kwa kutegemea fedha zinazotokana na vyanzo vya ndani.

Walitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana walipokuwa wakitoa maoni yao kuhusiana na msimamo wa Rais Samia alioutoa juzi kuhusu mikopo ambayo Serikali yake imekuwa ikikopa.

Alisema Serikali yake itaendelea kukopa kwa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nchi.

Akizungumza Ikulu juzi jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha mwisho cha Reli ya Kati kutoka Tabora kwenda Kigoma, Rais Samia alisema:

“Tunakopa ili tujenge leo kwa maendeleo endelevu ya leo na baadaye, kwa hiyo kila pale tunapohisi pana faida tutaendelea kukopa, kwa hiyo waseme awamu hii imekopa sana, lakini waseme pia kwamba awamu hii ndiyo iliyojenga sana pia.”

Mmoja wa wasomo hao, Abdallah Hamis, alisema Rais Samia yupo sahihi, kwani ili nchi iweze kutekeleze miradi mikubwa ni lazima ikope.

“Anakopa kujenga nchi, kosa liko wapi? Miradi inayotekeleza na fedha hizo inaonekana waziwazi na ili jampo la kupongeza,” alisema na kumpongeza Rais Samia kwa Serikali yake kuendelea kuaminiwa na taasisi za fedha pamoja na wadau wa maendeleo.

Alisema mkopo mbaya ni ule unaoishia mdomoni. Lakini hapa nchini kila sehemu tunaona miradi mikubwa inajengwa. Hatujasikia mfanyabiashara akilalamika kwamba akaunti yake imefungiwa. Sasa Watanzania wanataka nini?”Alihoji.

Alifafanua kwamba mkopo usiokuwa na tija ni ule ambao haujulikani unafanya nini. “Leo hii nchi ina kilometa za reli zaidi 2000 zilizojengwa kwa kiwango cha SGR. Uliona katika nchi gani za Afrika?” alihoji.

Mkurugenzi Mkuu TRC, Masanja Kadogosa, akizungumza juzi alisema kukamilika kwa ujenzi wa kipande hicho kutaifanya Tanzania kuwa nchi yenye reli ndefu ya SGR barani Afrika.

“Hakuna nchi yoyote barani Afrika ambayo inatarajia kujenga au ilishajenga reli ya SGR yenye kilometa 2,102,” alisema Kadogosa.

Msomi mwingine, Anna Joachim alisema ili nchi iendelee kuaminika na kukopeshwa, lazima iwe na sifa ya kulipa madeni. “Serikali yetu inaendelea kulipa madeni tunayokopa na tunazidi kukopa ili kujenga nchi.

Miradi inayojengwa leo sio kwa maslahi ya viongozi, ni kwa maslahi ya kizazi kijacho na hiyo hiyo miradi itarudisha fedha hizo,”alisema.

Alisema kwa hulka binadamu anataka kulaumu lakini wanasahau kusema mazuri yanayofanywa na Serikali. “Lakima tuwe na utamaduni wa kupenda nchi yetu. Tusipo penda nchi yetu nani mwingine atakuja kusema yanayofanyika?” alihoji.

Alitoa mwito kwa Rais Samia kutovunjika moyo na badala yake kuendelea kukopa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nchi.

000000000000000000000000000000000000
ANCHOR

Samia kushuhudia ujazaji
maji Bwawa la Nyerere leo