Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Steven Wasira, amewataka Wenyeviti wote wa chama hicho nchini, kuiga ubunifu uliofanywa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge.
Ambaye ameendelea kuiboresha ofisi ya chama hicho mkoani humo, na kusaidia wananchi kusikilizwa na kutatuliwa kero zao pindi wanapofikankatika ofisi hizo.

Wasira amezungumza hayo kwenye mkutano wa ndani na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakati alipokuwa kwenye ziara ya siku tatu mkoani Mbeya, amesema Mkoa huo umeonesha njia kwa mikoa mingine kuboresha mazingira ya ofisi zao na kutenga muda wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Pia amesema, kazi ya CCM ni pamoja na kutatua matatizo ya wananchi,hivyo ni vyema viongozi wakawa karibu na wananchi ili kujua matatizo yao kwa urahisi,huwezi kutatua matatizo ambayo hauyajui,hujayasikia na wahusika hujaonana nao.
Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Patrick Mwalunenge,amesema yeyote anayetaka kugombea nafasi ya uongozi katika uchaguzi mkuu, kupitia chama hicho kwa Mkoa wa Mbeya kigezo cha kwanza ni yule anayeweza kushughulika na matatizo ya watu.
Amesema msingi na uhalali wa CCM kuendelea kuingoza unatokana na viongozi wanao tatua shida na changamoto za wananchi katika maeneo yao na kusema kuwa haiwezekani kiongozi akashughulika na ‘tumbo lake’ badala ya kutatua shida za watu.

Aidha amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mbeya kuwa, katika uchaguzi watahakikisha viongozi watakao pita katika nafasi za uongozi hawatatokana na rushwa na majungu, bali kwa vigezo vinavyokubalika katika jamii.
Huku akisema kuwa CCM katika Mkoa wa Mbeya imejijengea sifa nzuri kwa wananchi wake kwa kufanya siasa za kuwafikia wananchi katika maeneo yao na si vinginevyo.

More Stories
NACTVET yawahakikishia wadau, usimamizi thabiti wa ubora wa elimu ya Ufundi na Amali
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,yajizatiti kuboresha uwezo wa Mawakili wa Serikali
MSD:Serikali inatekeleza mpango uchujaji wa damu