Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Promosheni ya mtoko wa kibingwa imewarahisishia washindi wake kuja jijini Dar es Salaam na kurudi kwa usafiri wa ndege kutoka katika mkoa mbalimbali kuja kuutazama mtanange wa simba dhidi ya yanga.
Mtanange huo unatarajiwa kufanyika tarehe 16 Machi katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mteja atakayeshinda tiketi hiyo ataweza kupata siti ya VIP.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa kampuni ya BETIKA, Juvenalius Rugambwa, amesema mpaka sasa tayari baadhi ya mabingwa kutoka mikoani waliojishindia tiketi za ndege kuja kwenye mtoko wa kibingwa wamepatikana.
Amesema tarehe za droo za wiki hii ni tarehe 27, 28, 1 na 3.
“Washindi wanapatikana kupitia droo za kila wiki na kila wiki Betika tunangaza washindi zaidi ya 10”
Pia amefafanua jinsi ya kushiriki kwenye droo hiyo ili kuweza kupata ushindi.
“Jinsi ya kushiriki ni beti mikeka 5 kila siku na hakikisha kila mkeka unabeti kwa dau la kwanzia 500 na kuendelea. Unaweza ukabeti kwenye website yetu ya www.betika.co.tz au unaweza ukapiga *149* 16# “
“Mkeka wako uchanike au usichanike moja kwa moja unaingia kwenye droo ya mtoko wa kibingwa ambayo itakupa furesa kuja jijini Dsm kwa usafiri wa ndege kwenda na kurudi kuja kushuhudia mtanange wa Simba Vs Yanga April 16.”
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM