January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Washindi wa “Magifti Dabodabo’ waanza kupatiwa zawadi zao

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

DROO ya kwanza ya kampeni ya ‘Magifti Dabodabo’ imefanyika juzi ambapo washindi 21 wamepatikana kutoka mikoa mbalimbali na kupatiwa zawadi zao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema katika droo ya kwanza wamewapata washindi mbalimbali wakiwemo wa safari ya Dubai, Zanzibar, vifaa vya ndani na fedha taslimu.

Alisema washindi wa kampeni ya Magifti Dabodabo’ msimu huu wa mwisho wa mwaka wanapata fursa ya kuchagua wenza wao au watu wa karibu kwa ajili kuwapendekeza kupata zawadi.

“Tumefanya droo ya kwanza na kupata washindi wa zawadi mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, kampeni ya Magifti Dabodabo inatoa fursa kwa washindi kuchagua wenza wao au watu wa karibu kujidhindia zawadi kama zao,” alisema.

Msemaji wa Kampeni ya Magifti Dabodabo, Haji Manara alisema Tigo imezindua kampeni hiyo kwa ajili ya kurejesha wanachokipata kwa jamii.

Alisema washindi walipatikana kutokana na kufanya miamala mbalimbali ikiwemo ya Tigo Pesa, kununua salio la muda wa maongezi na umeme wa luku.

Aliwataka wateja wa Tigo kuendelea kutumia mtandao huo kufanya miamala mbalimbali kuhakikisha wanaingia katika droo zingine kwani kampeni itaendeshwa kwa muda wa siku 80 nchi nzima.

“Tunawaomba wateja kuendelea kufanya miamala mbalimbali ili kuingia katika droo ya Magifti Dabodabo, kampeni itaendeshwa kwa muda wa siku 80 na kuna zawadi kubwa ya magari mawili mapya,” alisema Haji.

Naye mshindi wa safari ya kwenda Dubai, Meshack Ngowi wa Dar es Salaam, alisema amefurahia kupata fursa ya kwenda nchini humo na anatarajia kuongozana na mkewe.

Alisema alipata fursa hiyo kutokana na kutumia mara kwa mara miamala mbalimbali ya Tigo Pesa na kwamba anaamini safari hiyo itafungua fursa ya kushinda zaidi.

“Nimefurahia kupata fursa ya kushinda safari ya kwenda Dubai ninatarajia kuongozana na mke wangu, ninaamini ushindi huu utafungua milango ya kushinda zawadi kubwa zaidi, hivyo ninaishukuru Tigo kwani malengo yangu yanakwenda kutimia” alisema.