January 20, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Washindi 100 wa BETIKA washuhudia ‘Live’ Mechi ya Simba na Yanga

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Washindi 100 wa mtoko wa kibingwa wa BETIKA wamefika katika uwanja wa mkapa jijini Dar es Salaam, kushuhudia Derby ya simba na yanga

Afisa Uhusiano wa kampuni ya BETIKA, Nelson Pius amesema Washindi hao 100 waliotoka katika mikoa mbalimbali na kutua katika uwanja wa ndege jana, ambapo walilala katika Hotel yenye Hadhi ya Nyota 5.

Wachezaji hao walipelekwa uwanjani hapo kwa king’ora ambazo ni moja ya huduma zilizotajwa na BETIKA kwaajili ya wateja wao ambao wamebeti kupitia kampeni ya mtoko wa kibingwa.

Pius amesema mabingwa wa promosheni ya mtoko wa kibingwa kushuhudia mechi hiyo wamekua wakiifanya mara kwa mara huku kila msimu idadi ya mabingwa hao kuongezeka.