Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
WASANII takribani tisa hapa nchini wa muziki wa Bongofleva watapokea tuzo wiki hii kwa kuvunja rekodi ya kuwa na wasikilizaji wengi Boomplay 2021.
Tuzo hizo maarufu kama ‘Boomplay Plaques’ hutolewa mara moja kila mwaka ili kutambua jitihada za wasanii wanaofanya vizuri kwenye App ya Boomplay.
Hii ni mara ya pili kwa tuzo hizo kutolewa ambazo ni mahususi kwa wasanii ambao wameendelea kufanya vizuri kupitia kazi zao za muziki ndani ya mwaka mmoja uliopita.
Meneja Mkuu wa Boomplay Tanzania, Natasha Stambuli amesema, Wasanii kama Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Rayvanny, Nandy, Mbosso, Zuchu, Aslay na Darassa ni baadhi ya wasanii ambao wameendelea kuvunja rekodi kupitia Boomplay, hivyo ni furaha kwao kuwatambua.
Stambuli ameongeza, vigezo vilivyotumika kuchagua wasanii ni pamoja na wingi wa usikilizwaji (streams) wa wimbo wa msanii husika, albamu na usikilizwaji unaotokana na ujumla wa nyimbo za msanii. Takwimu za washindi zimechukuliwa kuanzia mwezi Novemba 2020 hadi Mei 2021.
%%%%%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio