Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Sauti za baadhi za viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zimesikika wakisikitishwa na hali ya makamanda wenzao kujifungia ndani huku wakiwaacha viongozi pekee wakiwa barabarani tayari kwa maandamano
Kwa mujibu wa sauti hizo zimesikika zikisema “Habari za asubuhi makamanda hapa magomeni mapipa hali ni shwari kabisa hakuna polisi yoyote hapa ambaye nimemuona wala hakuna gari lao lolote ambalo nimeliona”
“Kwahiyo mpaka muda huu wa saa 2:30 hali ni shwari ila watu siwaoni sijui mmejificha wapi na wala sijui mpo wapi”
“Mnazi mmoja napo ni kweupe kabisa hakuna gari la polisi wala viashiria vyovyote vile vya polisi labda wawe askari kanzu nimemaliza kufanya patrol kwenye hii njia yangu ambayo nipo ya magomeni kwenda mnazi mmoja.
“Sasa narudi magomeni kwenye kituo changu, makamanda tokeni ndani acheni kulala” zimesikika sauti hizo
Kwa ujumla Hali ilivyo asubuhi ya leo Jumatatu Septemba 23, 2024 eneo la Ilala Boma, jijini Dar es Salaam wameonekana Polisi wa kutuliza ghasia wakiwa wametanda kudhibiti maandamano ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
yanayolenga kuishinikiza Serikali
kuchukua hatua dhidi ya utekaji na
upotevu wa watu nchini.
Septemba 11, 2024 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, yakiwemo ya makada wake, lakini Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku.
More Stories
Serikali yahimiza wananchi kutembelea vivutio vya utalii
Magunia ya kufungia tumbaku yakamatwa
Madereva 16,Mwanza wafungiwa leseni ya udereva