Na Irene Clemence
KANISA la Waadventista Wasabato Tanzania limetenga kiasi cha shilingi million 100 kwa ajili ya kuinga mkono Serikali ya Awamu ya tano katika mapambo dhidi ya virusi vya Corona (COVID-19).
Fedha hizo zitatumika kununua vifaa tiba mbalimbali ambavyo vitatolewa katika hospitali za Serikali bure. Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadvest Wasabato Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania, Mark Malekana jijini Dar es Salaam.
Amesema, kanisa hilo kupitia Shirika la Maendeleo na Misaada wakati wa maafa (ADRA) limejizatiti kushirikiana na serikali katika kupambana na virusi vya Covid-19.
“Tumekuwa tukitoa misaada mara kwa mara mfano tulitoa Arusha na leo tumetoa hapa wilaya ya Temeke,leo tumetoa gloves, vitakasa mikono boksi 182, barakoa boksi 45 na vitu hivyo vimegharimu thamani ya shilingi milioni 8,” amesema Mchungaji Malekana.
Amesema vifaa ambavyo wamekuwa wakivitoa vimekuwa vikitengenezwa hapa nchini, lakini pia wamekuwa wakitoa elimu ya namna gani ya kujikinga na maambizi hayo. Amesema utoaji wa vifaa hivyo hauta bagua watu na imani fulani badala yake vitatolewa kwa watu wote wenye mahitaji ili kuisaidia nchini kupambana na janga hili.
Naye Famasia wa Wilaya ya Temeke, Grace Ntangu ambaye alimuwakilisha Mganga Mkuu wa Temeke alilishukuru Kanisa ilo kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano ya ugonjwa huo.
Pia aliomba mashirika na watu mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali dhidi ya mapambano na ugonjwa huo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa