December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wapatiwa mafunzo ya uendeshaji kesi za wanyama pori

Na George Mwigulu,Timesmajiraonline, Katavi .

MAJAJI ,Mahakimu , Waendesha mashitaka na wapelelezi wanapatiwa mafunzo ya siku tano yanayolenga kuwapatia ujuzi na kubadilishana uzoefu.

Mafunzo hayo yanahusu upelelezi ,ukamataji ,upekuzi ,uendeshaji wa mashauri na uandishi bora ,utoaji adhabu katika mashauri ya wanyama pori pamoja na sheria za Kimataifa za wanyama pori na mali asili za mistu .

Mafunzo hayo yanayofanyika Mjini Mpanda Mkoa Katavi yalifunguliwa na Jaji Donstan Ngunguru na yamewashirikisha washiriki na viongozi kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (UA) PAMS Foundation na Mahakama kuu ya Tanzania .

Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni Majaji , wa Mahakama kuu Mahakimu , maafisa wa kutoka ofisi za mashitaka ,jeshi la polisi ,mamlaka ya kuthibiti na kupambana Dawa za kulevya na kikosi cha kudhibiti ujangili mafunzo hayo yakiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa makubaliano kati ya UA na PAMS Foundation ya kuwajengea uwezo wadau wote katika mnyororo wa utoaji haki hapa nchini .

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Jaji Donsta Ndunguru amesema makundi hayo yameshirikishwa kwenye mafunzo hayo kwa kuwa kila kundi lina wajibu wake katika kuhakikisha Mashauri yanakwenda vizuri Mahakamani na ndio msingi wa kuwakutanisha wadau hao kwa pamoja .

Amebainisha kuwa mashauri ya wanyama pori sasa hivi yanaweza kuvuka mpaka nje ya nchi hivyo ni lazima upelelezi wa mashauri hayo uwe ni wa hali ya juu na ndio maana wanawapelelezi kwenye mafunzo hayo na waendesha mashitaka lazima wajuwe mbinu mbalimbali

Jaji Ndunguru ameeleza unaweza kukakuta nyara zimetokea Tanzania lakini zimekamatwa nje ya mipaka yetu ya nchi kama kutakuwa hakuna wataalamu wakufatilia mambo haya itakuwa vigumu kuweza kufatkiwa mashauri mahakamani ndio maana wameona kuwa na umuhimu wa uwelewa wa pamoja .

Amefafanua kuwa uhifadhi wa Taifa hauja anza sasa hivi kwani ulikuwepo toka wakati wa asisi wa Nchi hii ambao waliona umuhimu wa kuwepo kwa uhifadhi kwani walitambua umuhimu wa hizi rasilamali za pori kwa uchumi wa taifa hili.

Hakimu Mkazi Mkuu Patrisia Kisinda ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa chuo cha mafunzo ya uongozi wa Mahakama Lushoto amesema chuo cha uongozi wa Mahakama kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya Kierikali ya PAMS Foundation wameweza kuandaa mafunzo hayo kwa kuwafikia makundi hayo .

Amefafanua kuwa wameamua kufanya mafunzo hayo kwa kuwa eneo lenyewe la wanyama pori ni eneo nyeti kwa kiasi kikubwa sana linachangia katika kukuza uchumi wan chi na kwasababu wameona kuna changamoto katika undeshaji wa mashauri hayo kwa ajiri ya kutafuta njia bora ya undeshaji wa mashauri hayo .

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ambaye ni mwendesha mashitaka wa kutoka ofisi ya Mashitaka Katavi Abron Bundala amesema kuwa mafunzo hayo yamefika kwa wakati muafaka kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la ujangili hapa nchini kwa sasa .

Wanatarajia baada ya mafunzo watanufaika kwa kuweza kuwa na uwezo zaidi wa kuendesha kesi kwa manufaa ya Taifa na kwa ulinzi wa wanyama pori wasiendelee kupotea zaidi kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo .