Na Irene Fundi, TimesMajira Online
WALIMU saba na wafanyabiashara watatu wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuvujisha mitihani ya darasa la saba mwaka 2022.
Watuhumiwa hao, walimu ni Jonson Ondieka, Elinami Sarakikya, Joyce Nkomola, Lloyd Mpande, Ronald Odongo na Dorcas Muro, Alcheraus Malinzi na wafanyabiashara ni Patrick Chawawa pamoja na Theresa Chitanda.
Wakili Mkuu wa Serikali, Nasoro Katuga akiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo alidai kuwa Malinzi anatuhumiwa kwa kosa la kutengeneza nyaraka za uongo za Serikali kwa kughushi nyaraka za mtihani wa somo la uraia na maalifa ya jamii huku akiaminisha kuwa umetungwa na Balaza la Mtihani.
Pia, Katuga amedai kati ya Oktoba 2 hadi 3 mwaka huu , watuhumiwa walitumia mitandao ya kijamii ikiwemo telegram na WhatsApp kusambaza mitihani hiyo.Baada ya washitakiwa hao kuulizwa mbele ya mahakama kuhusu tuhuma hizo wamekana kutenda makosa hayo.
Hata hivyo, Katuga ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo huku wakiendelea kukamilisha upelelezi na kuwatafuta watuhumiwa wengine.
Kesi hiyo imehairishwa hadi Novemba 2, 2022 kwa ajili ya kutajwa, ambapo washitakiwa wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja na kusaini bondi ya Sh milioni tano.
More Stories
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba