January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanufaika: WCF imetufuta machozi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

WANUFAIKA wa fidia inayotolewa na WCF, wametoa ya ‘moyoni’ mbele ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, kwa kile walichokiita Mfuko huo umewafuta machozi.

Wakitoa ushuhuda Novemba 2, 2023, katika kikao kazi baina ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Wahariri wa vyombo vya habari, kuelezea utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya Mfuko huo, miaka 8 tangu kuanzishwa kwake.

Beauty Jackson Letema, ni mnufaika wa WCF, yeye ni mama mjane ambaye alifiwa na mumewe katika ajali wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri wake.

“Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, lakini pia naishukuru WCF, mume wangu alipofariki aliniacha na watoto watatu na ujauzito, WCF walianza kunihudumia mimi na watoto wangu hao watatu na kisha huyu mwingine, Mimi sikuwa na kazi yoyote ya kufanya, WCF wanatuhudumia mimi na watoto, tunavaa, tunakula na pia watoto wangu wanasoma bila shaka yoyote, kwakweli wamenifuta machozi.” Amesema

Kutokana na manufaa anayoyapata kutoka WCF, Mnufaika huyo aliwahimiza waajiri kujisajili na mfuko ili wafanyakazi wanapopatwa na madhila wakiwa kazini, basi Mfuko utakuwa mfariji wao.

“Wito wangu kwa waajiri, WCF ni mfuko wenye faida sana, kama mimi mume wangu alivyofariki na mwajiri wake angekuwa hajajisajili WCF, maisha yangekuaje?  Natoa wito kwa waajiri wajiunge na WCF.” Amesisitiza Beauty.

Mnufaika mwingine ni Halima Sheikh, wakati akitekelza jukumu lake kama dereva wa bus la abiria, Super Feo, alikatika mkono baada ya bus alilokuwa akiliendesha kupinduka.

“Baada ya kupoteza mkono na kupata ulemavu wa kudumu, WCF imekuwa ikinilipa fidia kila mwezi, malipo yananisaidia mimi na familia yangu, nimeambiwa nitalipwa maisha yangu yote, hakika nafarijika sana.” Amesema.

“Kwa kifupi naishukuru sana Serikali kwa kuanzisha WCF, Mfuko una manufaa makubwa sana, ninajitegeema asilimia 100, namshukuru Mkurugenzi Mkuu wa WCF na timu yake, Mfuko umenipatia matibabu vizuri sana hadi kupona,  maisha yangu yanaendelea.” Amesema Mnufaika mwingine, Bw. Hassan Sima Jambau, aliyekuwa mtumishi wa Televisheni ya Taifa, TBC.

Mnufaika wa fidia itolewayo na WCF, Bi. Halima Sheikh, akitoa ushuhuda mbele ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam, Novemba 2, 203.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma akifurahia jambo na mmoja wa watoto ambao wanapokea fidia kama wategemezi baada ya kumpoteza baba yao, Jackson Letema.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma akiwasalimia wanufaika wa fidia inayotolewa na WCF mara baada ya kikao hicho.

Beauty Jackson Letema, mnufaika wa WCF, akitoa ushuhuda mbele ya Waandishi wa habari

Bi. Halima Sheikh

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kushoto), akiteta bjambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Thobia Makoba.

Mwandishi wa habari mwandamizi na Mhariri, Bw. Joe Nakajumo akiwa mwenye hisia wakati akisikilzia ushuhuda wa wanufaika wa fuidia.

Baadhi ya washiriki

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile (kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano WCF, Bi. Laura Kunenge.

Mkurugenzi Mkuu (WCF), Dkt. John Mduma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanufaika wa fidia inayotolewa na WCF.