


Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WALENGWA wa Mfuko wa (TASAF),wameiomba Serikali kuendelea kusaidia kaya masikini Ili ziweze kuimarika kiuchumi na kumudu maisha yao ikiwa ni pamoja na kulea familia zao.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya Kimataifa ya wakulima maarufu kama Nane Nane Agosti Mosi mwaka huu yanayoendelea jijini Dodoma,walengwa hao pamoja na kumshukuru Serikali kwa namna ilivyowasaidia lakini Bado wameomba kuwezeshwa zaidi.
Palesta Nyanda Mkazi wa Dar ES Salaam ambaye ni mhitimu wa TASAF amesema kupitia Mpango wa TASAF ameweza kuimarika kiuchumi kwa kufanya miradi kutokana na uwezeshwaji wa TASAF.
“Kabla sijaingia TASAF nilikuwa mdhaifu na kukabiliwa na magonjwa ,lakini nilikuwa naokota dampo ,maisha yangu yalikuwa magumu sana pia nilikuwa nimepooza ,lakini baada ya kuingia kwenye Mpango nimeanzisha biashara zangu ,watoto wangu wanaosoma yupo wa chuo ,kidato Cha nne na kidato Cha pili.”alisema Nyanda
Amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye mwaka Jana katika maonesho ya Nane Nane alimwezesha lakini pia amejengewa nyumba na Serikali lakini pia kupitia TASAF pamoja na biashara nyingine anauza dawalishe zinazotibu sukari,kupooza huku akisema dawa hizo zimemsaisia hata kutibu naradhi yaliyokuwa yakimkabili.
Pili Selemani mkazi wa wilaya ya Bahi ameiomba serikali kuongezs uwekezaji kwenye mfuko huo ili kusaidia kuwaondoa watu kwenye ufukara katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Pili amesema mfuko huo umekuwa msaada mkubwa sana kwa jamii kutomana na kwamba umewatoa watu wengi kutoka kwenye umaskini na kuwavusha kufikia hatua ya kula milo mitatu.
“Tunaiomba serikali iendelee kuwekeza katika mfuko wa TASAF unasaidia jamii kuwa wajasiriamali kutokana na fedha ambazo wamepewa kujikimu wao na familia zao,”amesema Pili.
Akisimulia TASAF ilivyomuinua kimaisha alisema awali alikuwa hana uhakika wa kula lakini hivi sasa kupitia fedha anazopewa na TASAF amefanikiwa kuanzisha ujasiriamali ambao unsaidia kusomesha watoto”,alisema Pili.
Naye Mariam Kassim kutoka wilaya ya Kusini Unguja Zanzibar ambaye pia ni mlengwa wa TASAF,amesema mfuko huo umechangia kwa kiasi kikubwa kumtoa katika umaskini na kupelekea kuwa mjasiriamali wa vitu mbalimbali ambavyo humpatia kipato.
Kutokana na hilo alisema kupitia maonyesho ya nanenane amewataka wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo kujifunza namna ya kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo vitawainua kiuchimi.
Amesema pamoja na serikali kuwadia fedha kutoka mfuko wa TASAF wanaiomba iwasaidia pia vitendea kazi ambavyo vitawasaidia kufanya shughuli za ujasiriamali katika maeneo mbalimbali.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi