Na Esther Macha, Timesmajira Online, Kyela
WANUFAIKA wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia Mpango wa Kususuru Kaya Maskini wilayani Kyela mkoani Mbeya wamewaasa wanufaika wa mfuko huo wanapopewa msaada na serikali wajue kuweka akiba pamoja na ruzuku wanazopewa kwa ajili ya kujikwamua kimaisha na kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mmoja wa wanufaika wa TASAF, Upendo Chibongwe ambaye ni mkazi Ikama Wilaya ya Kyela amesema kuwa ipo haja kwa wanufaika wa mfuko huo kuona umuhimu wa kuweka akiba pindi serikali inapowasaidia ili waweze kujikwamua kimaisha hususani kusomesha watoto wao pamoja na mahitaji mengine ya msingi.
Hata hivyo amesema kuwa akiwa na familia ya watoto watano mume wake alimuaga kuwa anaenda kutafuta maisha nje ya nchi lakini cha kushangaza hakuweza kurudi tena kuangalia familia yake.
“Nikiwa kijijini huku ambako mume wangu alinirudisha kwa ahadi kuwa anaenda kutafuta maisha nilianza kupata shida na watoto na maisha kuwa magumu ndipo serikali iliponiona na kuingizwa kwenye Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) na kupatiwa fedha ambazo nilinunua kuku na kuanza kufuga ambapo ufugaji huu ndio umenipa nguvu nasomesha watoto wangu waliopo kwenye vyuoni na shule za msingi “amesema mwanamke huyo.
Kwa upande wake Naomi Msakwa amesema kuwa wananchi wanatakiwa fedha za TASAF kuzitumia vizuri na kufanya miradi mbali mbali na sio kudharau kuwa ni fedha ndogo .
“Tusiseme fedha hizi ni ndogo kwani kwa walengwa walioweka malengo zinasaidia ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto na kupata mahitaji mbali mbali ya kifamilia ,nawaasa walengwa wengine kuzitumia fedha za TASAF kujikomboa kimaisha maana mfano mimi nilikuwa na maisha magumu sana kabla ya kuingia kwenye mpango huu hivyo siwezi kudharau fedha hizi zimenitoa kwenye umaskini mkubwa niliokuwa nao kwa hizi hizi fedha nitazidi kuboresha miradi yangu ninayofanya kupitia fedha hizi za TASAF”amesema mkazi huyo wa Ndola Msakwa.
Kwa upande wake Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya maskini Wilaya ya Kyela(TASAF) ,Pili Busenghwa amesema kuwa ana vijiji 11 ambavyo vipo kwenye mpango na kati ya vijiji hivyo wamefanikiwa kutembelea vijiji sita ambapo walengwa wana shughuli mbali mbali ambazo wanafanya ambazo ni kusuka mikeka ya kinyeji , ufugaji wa kuku , nguruwe ,na Ng’ombe , kukamua mawese.
Aidha Mratibu huyo amesema kuwa wana walengwa 6,530 na kusema kwamba katika wilaya ya kyela wamefurahia mpango huo kwani walengwa walio wengi kabla ya kuingia kwenye mpango walikuwa na hali duni za kimaisha lakini hivi sasa hali zao za kimaisha zimeimarika kutokana na walengwa kuanzisha shughuli mbali mbali za ujasilimali za kuwaingizia kipato.
“Lakini pia katika kuhakikisha tunasaidia kaya za walengwa ambazo zina watoto wanaosoma mpango huo wa kunusuru kaya maskini wameweza kuwaandikia barua wanafunzi 10 za kuwatambulisha kwenye bodi ya mikopo ili waweze kupata mikopo na kusoma “amesema Mratibu huyo.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best