December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanufaika TASAF wakuza mitaji
kupitia ajira za muda

Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOnline, Makambako

WANUFAIKA 53 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) walioshiriki ujenzi wa barabara ya kilometa 7.2 kupitia utaratibu wa ajira za muda katika Kijiji cha Kiumba Halmashauri ya Mji Makambako, mkoani Njombe kwa wameanzisha miradi mbalimbali ya kuwaingizia kipato kupitia ujira waliokuwa wakilipwa.

Barabara hiyo inaunganisha mitaa mitatu ambayo ni Makatani, Kiumba na Muungano.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Kijiji cha Makatani, Samson Ally (62) ambaye alipewa jukumu la kusimamia mradi huo

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Ally amesema walengwa hao wa mpango wa TASAF kupitia kipato walichokuwa wanalipwa wengi wameweza kuongeza mitaji kwenye miradi yao, hivyo anaishukuru TASAF kwa kuendelea kutatua shida za wananchi.

“Kwa kwa kweli tunashukuru sana TASAF walengwa wote walioshiriki ujenzi wa barabara hii kupitia ajira za muda wameazisha miradi ikiwemo ya ufugaji kuku, mbuzi na nguruwe ambayo inawasaidia kuingiziza kipato,” alisema Lukogera.

Amesema kupitia miradi waliyoanzisha inawapa uhakika wa kula milo mitatu kwa siku, kununa mahitaji ya shule watoto na huduma za afya

Barabara iliyojengwa na wanufaika wa TASAF

Alitaja miongoni mwa kazi walizokuwa wakifanywa wakati wa ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 7.2 kuwa ni pamoja na kung’oa visiki.

Amesema utekelezaji wake ulianza Novemba, 2020 ambapo barabara hiyo inapita kijiji chote cha Kiumba na kwa sasa wanamalizia ujenzi wa maravati matatu ili iweze kukamilika kwa asilimia 100.

Akizungumzia faida ya barabara hiyo mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Makatani alisema barabara hiyo inarahisisha usafirishaji wa mazao mbalimbali na ni kiunganishi cha mitaa ya kijiji hicho.