January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanne wafariki ajali ya ndege kugongana angani

Na Mwandishi Wetu

WATU wanne wamefariki baada ya helikopta mbili kugongana angani karibu na Seaworld kwenye pwani ya Australia ya Gold Coast .

Abiria wengine tisa waliokuwa ndani ya ndege hizo mbili wote walitibiwa majeraha, huduma ya ambulensi ya Queensland ilisema.

Abiria watatu – mwanamke na wavulana wawili – wamepelekwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya.

Ofisi ya Usalama wa Usafiri wa angani ya Australia (ATSB) imesema itachunguza.

Mgongano huo uliofanyika mwendo wa saa 14:00 kwa saa za huko (04:00 GMT) kando ya ukanda wa watalii unaojulikana kama Main Beach, takriban kilomita 75 (maili 47) kusini mwa Brisbane.

Gary Worrell kutoka idara ya polisi ya Queensland aliwaambia waandishi wa habari kwamba helikopta moja ilionekana kupaa huku nyingine ikitua.

Alisema vifo vya watu wanne na majeruhi watatu vilitoka katika ndege moja.

“Ni eneo gumu,” alisema. “Kutokana na eneo lilipo, kwenye ukingo wa mchanga, ilikuwa vigumu kupata huduma zetu za dharura kwenye eneo la tukio ili kulisimamia ipasavyo.