Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Kuelekea Kilele Cha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Leo Machi 3,2025, Watumishi Wanawake Wizara ya Madini wameungana na wenzao kutoka Mikoa ya Singida, Dodoma na Iringa kushiriki Kongamano la Kanda ya Kati linalohusisha Mikoa hiyo.
Kongamano hilo linalofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventional Center Jijini Dodoma likiongozwa na mada isemayo “Wanawake na Uongozi katika miaka 30 ya Beijing.

Mgeni rasmi katika Kongamano hilo ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda.
Kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kitafanyika Jijini Arusha, Machi 8, 2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo kwa Mwaka 2025 inasema ” Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji,”
More Stories
Wakazi Mahomanyika wamlilia Rais Samia kuingilia kati mgogoro wa ardhi
Dar kufanya kongamano maalum kuelekea maadhimisho ya siku ya Mwanamke Dunia
Sheria kuitambua maabara Tume ya Madini