Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbarali
WANAWAKE wilayani Mbarali, mkoani Mbeya wametakiwa kuwa sehemu ya kumsemea vizuri Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ili aweze kusonga mbele na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika kuwatumikia Watanzania.
Hayo yamesemwa jana na Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi, Mary Prisca Mahundi (pichani juu) wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wilaya hiyo.
Amesema kuwa wanahitaji kumuona Rais anafanya kazi katika mazingira tulivu . “Mh. Rais Samia akiwa Dodoma wakati anaongea na wanawake kwa niaba ya wanawake wa Tanzania alisema wanawake ni kama kajani cha chai unapotia kwenye maji moto kanazidi kukolea ukikaacha kanazidi kukolea ukikiacha mpaka chai inakuwa chungu ndo kama sisi wanawake mkitupa nafasi tunaonyesha uwezo na tunafanya kazi kwa kujituma” alisema Mhandisi Mahundi.
Hata hivyo Mhandisi Mahundi amesema kuwa Mama Samia amepewa nafasi ya Urais tunategemea mambo mazuri mengi wale ambao wanataka kumshika gauni ili asiende mbele tusiwaruhusu .
Mahundi amesema kuwa watakikisha wanawake wa Mkoa wa mbeya wanashikamana mahala popote na maeneo ya mikusanyiko katika shughuli zao lazima wamsemee vizuri Mama Samia.
Aidha Mhandisi Mahundi ametumia nafasi hiyo kuwahimiza Wanawake kuhifadhi mazingira ili kulinda vyanzo vya maji kwa kutumia nishati ya gesi sambamba na upandaji miti pamoja na kugawa miche ya miti ya parachichi, kukabidhi majiko ya gesi kwa kila mjumbe kupitia taasisi yake ya MaryPrisca Women Empowerment Foundation.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa umoja wa Wanawake wilayani humo,Zabibu Baharam amesema kuwa wanajivunia kuwa na naibu waziri mwanamke .
Akizungumzia kuhusu matumizi ya nishati ya kuni na mkaa Zabibu amesema Wanawake wamekuwa watumiaji wa kuni kwa kiasi kikubwa hivyo mpaka wamekuwa wakitumiwa uchawi majumbani mwao kutokana na macho mekundu.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba