December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake watakiwa kubuni miradi mbalimbali kukuza uchumi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wanawake hapa nchini wameaswa kuhakikisha kuwa hawajibweteki na kuridhika na Mali za familia pekee Bali wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanabuni miradi mbalimbali ambayo itaongeza uchumi

Hayo yameelezwa na Bi hyka Budah ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Somon Enterprise kutoka Jijini Arusha wakati akiongea na wanawake kwenye usiku wa tuzo za wanawake Arusha zilizofanyika hapo Jana

Hykal alisema kuwa wanawake wanatakiwa kuhakikisha Kila mara wanabuni miradi ambayo itaweza kuchochea maendeleo hata kama wana ndoa.

Alisisitiza kuwa wanawake hata wenye ndoa nao hawapaswi kukaaa nyumbani pekee Bali nao wanatakiwa kujishugukisha huku wakiwa wanahudumia ndoa zao ipasavyo

“Ni muhimu Sana kuweza kulinda na kutunza ndoa zetu lakini pia tuhakikishe kuwa tunazilinda Kwa kiwaeshimu wanaume zetu na pia haitoshi Tu Kila mwanamke sasa anatakiwa kuwajibika ipasavyo katika kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo

Akiongelea kiwanda chake alisema kuwa mpaka sasa kiwanda hicho kimeweza kuzaaa ajira nyingi na pia kimeweza kupambana na adui Umaskini

Alidai kuwa wameweza kuzalisha sabuni za Aina mbalimbali ambazo hapoo awali zilikuwa zinazalishwa nje ya mkoa wa Arusha huku nyingine zikiwa zinatoka hata nje ya nchi

“Tunashukuru kweli tumeweza kuzalisha sabuni za magari,za usafi,za kungarisha sakafu kama Tiles lakini na sasa tupo kwenye mchakato mzima wa kupandaa sabuni za mche kwani nazo tuna uwezo mkubwa wa kuzitengeneza tena kwa kiwango ambacho kina ubora wa kutosha”alisema

Katika hatua nyingine aliwashukuru waandaji wa tuzo za wajasiriamli Arusha kwa kuwa zimeweza kuwafanya wajasiriamli wengi kuinuka na kupata hamasa hasa ya kupiga hatua kwenye harakati zao za hapa na pale