Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wanawake nchi wametakiwa kutumia kauli mbiu ya siku ya wanawake kuwa kama dira itakayowasukuma kuingia kwenye uwekezaji na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo itakayosaidia kuinua uchumi wao na kuwaondoa kwenye changamoto zinazowakabili za umaskini na kidharauliwa
Ushauri huo umetolewa na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea viwatilifu kanda ya mashariki wakati wakimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa mamlaka afya ya mimea na Viwatilifu TPHPA Profesa Joseph ndunguru kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa akina mama waliojifungua katika hospitali ya bunju Jijini Dar es Salaam sambamba na kugawa Miche 60 ya matunda kwenye za msingi na sekondari.
Dkt Sasamalo amesema Jitihada na ni wajibu wao TPHPA kutunza mazingira, afya ya binadamu na wanyama.
Akizungumza meneja wa Kanda ya mashariki Dkt Mahamudu Sasamalo amesema kauli mbiu ya siku ya wanawake inayobeba ujumbe wekeza Kwa mwanamke Kwa maendeleo ya kitaifa na ustawi wa jamii ni dira ambayo wanawake wakiitumia viziri inaweza kuwaondoka kwenye changamoto.
Dkt Sasamalo ambaye pamoja na ujumbe wake Kwa Kanda ya mashariki wamemuakilisha mkurugenzi mtendaji wa TPHPA Pro Ndunguru anasema kama wadau muhimu katika sekta ya kilimo na wasimamizi wakuu wa afya ya mimea na viwatilifu wanahimiza wanawake kuwekeza katika kilimo kwani kwa sasa ndio kwenye fursa nyingi ambazo watu wengi hawazitambui
Aidha akizungumzia kuhusu usalama na faida ya wanawake kuwekeza katika kilimo ni kutokana na mikakati ya mamlaka TPHPA katika kustawisha sekta ya kilimo na tayari serikali imetoa fedha nyingi Kwa ajili ya viwatilifu salama kwa uhai wa minea lakini pia kukabiliana na visumbufu wa mazao.
Akizungumzia kuhusu zoezi la ugawaji Miche ya matunda kwa shule za msingi na sekondari Dkt Sasamalo amesema lengo la Mamlaka na mkurugenzi wa mamlaka hiyo Prof Ndunguru ni kutimiza ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutaka watanzania kutunza mazingira kwa kuoanda miti Kwa wingi
“Lakini pia Kama TPHPA tumeamua kutoa miti ya matunda na haswa mashuleni kwa kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata hewa safi, kivuli na zaidi wapate matunda. Ameongea Dkt Sasamalo.
Akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa wawakilishi kutoka Kanda ya Mashariki ambao ulitenbelea na kukabidhi msaada wa taulo za kike Kwa akina akina mama walijifungua , pempers za watoto na sabuni Heleni Kimaro anaitaka jamii kujenga utamadumu wa kuwa na moyo wa kuwasaidia makundi ya wanawake wenye uhitaji hasa katika wodi za wazazi.
Kwa Upande wake Muuguzi Kiongozi wa Kituo cha Afya cha Bunju Ester Chacha amesema tangu kuanza wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo kilele chake ni Machi 8 jumla ya Watoto 41 wamezaliwa katika hospitali ya bunju huku Watoto wa kike wakiwa wengi zaidi kuliko Watoto wa kiume
TPHPA Kanda ya Mashariki inaunganisha Mikoa ya Pwani , Dar es salaam, Morogoro na Tanga imefanya maadhimisho ya wanawake kwa kushiriki shughuli mbalimbali iza kijamii kiwamo kutoa msaada na kupanda miche 60 ya matunda katika shule zashule ya secondary diplomasia, uhamiaji na shule ya msingi kiungani na sekondari, zoezi liliongozwa na meneja wa kanda hiyo Dkt Mahamudu Sasamalo.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi