December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake, waliochangia demokrasia kutambuliwa

Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Dar

Licha ya jitihada za wanawake kuchangia demokrasia nchini, lakini bado mchango wao haujathaminiwa,hali ambayo inafifisha jitihada hizo.

Hivyo Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake (WRIFOM),limezindua mradi wa kuwawezesha waandishi wa habari wanawake,kuibua wanawake waliofanya vizuri katika demokrasia,lakini mchango wao haujatambiliwa.Ili kuleta chachu katika na kubadili mitazamo hasi katika jamii.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo,uliofanyika Septemba 13,2024,jijini Dar-es-Salaam,mmoja wa waanzilishi wa WRIFOM, Chelu Matuzya, ameeleza kuwa mradi huo,unashirikisha waandishi wa habari wanawake 15, kutoka baadhi ya mikoa nchini.Ambao umelenga kuibua wanawake waliochangia demokrasia nchini.Pamoja na kubadili mitazamo hasi katika jamii juu uwezo wa wanawake katika kufanya mambo mbalimbali.

Chelu, ameeleza kuwa, mradi huo wa WRIFOM,unatarajiwa kuleta mabadiliko kwa kuibua na kutambua wanawake waliochangia katika demokrasia, huku ukileta mabadiliko chanya katika mitazamo ya jamii kuhusu wanawake katika siasa.

“Waandishi wa habari walioshiriki mradi huu, wanatarajiwa kuandika habari zitakazosaidia kuongeza usawa na kutoa motisha kwa wanawake wengine,”ameeleza Chelu.

Akizindua mradi huo,Mkuu wa Wilaya mstaafu(Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi),Betty Mkwasa, ameeleza kuwa changamoto zinazowakabili wanawake, kama vile mila, desturi, na mfumo dume, ambazo zinawazuia kujieleza hata katika mambo ambayo yanawahusu.

“Ninyi mliopata nafasi katika mradi huu,nendeni mkajitume na kuwaibua wanawake waliofanya mambo mazuri, na kuwaacha alama ya kudumu,”.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Dustan Kamanzi,amesema,licha ya jitihada na mchango wa wanawake katika demokrasia,haujathaminiwa ipasavyo, na mara nyingi hawapati nafasi stahiki.