Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Mwanza
Septemba 2,2024 katika mwalo wa Igombe, Kata ya Katale wilayani Magu, kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP. Wilbroad Mutafungwa.Ina ibuka hoja ya wanaume kuwatupia lawama wake zao,kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro katika ndoa.
Miongoni mwa walio hudhuria mkutano huo ni pamoja na Mzee Mali Msoga,ambaye anaeleza namna ambavyo wanaume wamekuwa wakishughulikiwa na sheria baada ya kuchukua hatua dhidi ya wake zao.
”Unapochukua hatua fulani kwa lile kosa ambalo mke wako amekufanyia, anakimbilia kituo cha Polisi, kisha Polisi wanakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria.Lakini wanawake, ndio chanzo cha matatizo kwenye ndoa,” amesema Msoga.
Kwa upande wake, Koplo wa Polisi (Cpl) Stella Liymo kutoka dawati la Jinsia na Watoto,ameitaka jamii kuacha tabia za kurusha picha za watoto waliotendewa ukatili,kwani kunawaharibia na kufifisha ndoto zao.
“Badala ya kusambaza picha za watoto waliofanyiwa ukatili. Wananchi toeni taarifa za watoto waliofanyiwa ukatili Polisi,ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahalifu,”amesema Clp.Stella.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Lutale Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Wilbroad Mutafungwa,ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutembelea visiwa na maeneo yaliyopo pembezoni mwa ziwa victoria kutoa elimu ya usalama wa majini, kusikiliza kero,changamoto, malalamiko na kupata ushauri kutoka kwa wananchi
”Jamii inatakiwa kujiepusha na matukio ya kikatili kwa wanawake, watoto na wanaume.Pia nyinyi mnaokaa pembezoni mwa Ziwa Victoria,tunawambia utajiri unakuja kwa kufanya kazi na siyo kwa njia za kishirikina, ushirikina ni njia mojawapo ya kujitafutia umasikini,” amesema Mutafungwa.
Aidha, kamanda Mutafungwa amewataka wavuvi na wananchi hao kuhakikisha wanazingatia usalama wao pindi wanapotumia mitumbwi katika kazi zao za majini,kwa kuvaa vifaa vya uokoaji ili kujiepusha na vifo vinavyoepukika pindi ajali inapotokea wakiwa ziwani.
Naye, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Magu, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Makame Haji,amewaomba wananchi, kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa haraka.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam