December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake wahasibu TANESCO washiriki kongamano Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online,Zanzibar

WANAWAKE Wahasibu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wameshiriki kongamano la kitaaluma la wanawake wahasibu linalofanyika katika hotel ya Verde Zanzibar.

Kongamano hilo la nne limefunguliwa jana na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Hemed Suleiman Abdallah akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ally Hassan Mwinyi.

TANESCO imefadhili kongamano hilo lengo likiwa ni kuwakutanisha wahasabu wanawake wa TANESCO na wataalamu wengine wa kada hiyo kutokana na makongamano kuwa sehemu mahususi ya kuzungumzia masuala ya kada ya husika.

Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar akihutubia katika kongamano la wahasibu wanawake wa Tanzania TAWCA lonalo endelea katika Hotel Verde visiwani Zanzibar
 Â