Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOline
KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi, Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) leo Machi 7, 2026 kimetembelea Hifadhi ya Ngorongoro na kutoa msaada kwa jamii ya Wamasai wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, mwakilishi wa Chuo cha Serikali za Mitaa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Tatu Lesso amesema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kuadhimisha siku hiyo muhimu inayotambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila tarehe 8 Machi duniani kote kwa lengo la kutambua mafanikio ya wanawake na kuhamasisha usawa wa kijinsia.

Katika ziara hiyo, chuo kimekabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa jamii ya Wamasai ikiwemo mahindi, unga, Mchele, sabuni za kufulia na kutoa ujumbe wa kuhamasisha elimu, afya pamoja na uwezeshaji wa wanawake na watoto wa kike katika maeneo ya hifadhi.
Wananchi jamii ya kimaasai ndani ya eneo hilo wamewashukuru wanawake hao na Chuo kwa ujumla kwa moyo wa kujali jamii, wakisema msaada huo utasaidia kuboresha maisha ya wanawake na familia zao.

Chuo cha Serikali za Mitaa kinaendelea kushirikiana na jamii mbalimbali nchini katika shughuli za kijamii zenye lengo la kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi.
Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka duniani kote kwa lengo la kutambua mafanikio ya Wanawake na kuhamasisha usawa wa kijinsia.
Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kitaadhimishwa kesho Machi 8, 2026 na kauli mbiu kwa awamu hii ni “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana; msingi jumuishi kufikia Dira 2050”.





More Stories
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi