February 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake Kisukuru kuwezeshwa kuku kujiinua kiuchumi

Na Hari Shaaban, Timesmajira Online,Ilala

DIWANI wa Kata ya Kisukuru Lucy Lugome,amesema mkakati alionao ni kuwawezesha kiuchumi Wanawake wa Kata hiyo kupitia vikundi vyao kwa kugawa kuku bure 50 ili waweze kukuza mitaji.

Lugome, amesema hayo Februari 19,2025,jijini Dar-es-Salaam katika mkutano wake na wananchi,ambapo amesema,”Wanawake wa Kisukuru kuna fursa inakuja kwa ajili ya kukuza uchumi kwa kushirikiana na wadau wangu wa maendeleo hivyo kuna utaratibu wakupata kuku bure kupitia vikundi vyenu tuwawezeshe kiuchumi,”.

Akizungumzia miundombinu amesema barabara za kisasa zinazojengwa Kisukuru kwa kiwango cha lami,sekta ya afya Serikali imeishaelekeza fedha kwa ajili kujenga hospitali ya kisasa yenye hadhi ya rufaa,ambapo fidia ya milioni 353 hekali tatu kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ipo tayari huku bilioni 5,nimeisha tengwa kwa ajili ya mradi huo.

Pia amesema madarasa matano shule ya sekondari yamekamilika kupitia fedha za UVIKO-19 ,matundu ya vyoo,ununuzi wa madawati 590, vyumba vitano vya madarasa shule ya msingi na uchimbaji kisima cha maji.