March 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake BUWASA watembelea wafungwa wanawake gereza la Bukoba

Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online,Kagera

Watumishi wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Bukoba ( BUWASA),wameadhimisha siku ya Wanamke Duniani kwa kutoa mahitaji mbalimbali kwa wafungwa wanawake wa gereza la Bukoba pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa matumizi ya maji safi na salama.

Akizungumza Machi 8,2025,Ofisa Uhusiano wa BUWASA Julieth Shangali,amesema wametoa taulo za kike,pampers kwa ajili ya watoto, ,sabuni,juisi ,soda,sukari pamoja na mahitaji mengine ya msingi.

Shangali,amesema pia wametoa elimu kuhusu matumizi ya maji safi na salama na umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji kwa sababu wanawake walio gerezani badae watakuwa ia na Wateja wa BUWASA.

Ofisa Utumishi kutoka BUWASA Rosada Mbowe,amesema wanatambua wanawake wanamahitaji mengi hasa wakiwa gerezani ndio maana wameamua kusherekea siku ya wanawake kwa kuwatemvelea wafungwa hao na kutoa msaada huo kwani Serikali haiwezi kufanya kila kitu.

“Tumefarijika,tumecheza ngoma nao,wametuimbia na tukatoa elimu, ,tumewatia moyo tukiamini kuwa siku moja watatoka na kuungana nasi uraiani,”amesema Mbowe.

Hata hivyo ametoa wito kwa taasisi nyingine kuwapelekea mahitaji ya kibinadamu wanawake walioko gerezani ili kuwapa faraja.

Kauli mbinu ya siku ya Wanawake Duniani mwaka huu inasema “Wanawake na Wasichana 2025, tuimairishe usawa haki na uwezeshaji”.