January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanasheria waombwa kusaidia kusimamia sheria, sera ulinzi wa taarifa

Na Mwandishi wetu , Timesmajira Online,Arusha

Wanasheria nchini,wameombwa kuisadia Serikali katika kusimamia sheria na utekelezaji wa sera mbalimbali za ulinzi wa taarifa nchini.

Huku jamii,ikihimizwa kushirikiana na viongozi wa kisekta, watetezi wa faragha na uhuru wa raia,ili kuwalinda watumiaji wa taarifa kwenye uchumi unaendeshwa na taarifa na kuwa na taifa linaloheshimu faragha.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahindi,Novemba 15, 2024 jijini Arusha wakati akifunga kongamano la anuai za kitaaluma lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS),kwa kushirikiana na privacy-professionals,ambapo amesema ulinzi wa taarifa ni wa kila mtu na sio wa Serikali pekee.

“Tunaishi katika enzi ambapo taarifa hutiririka katika tania, mipaka na mifumo ya ofisi kwa kasi,hivyo tunatarajia kushiriki kwa pamoja sisi Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kufika malengo tulijowekea,” amesema Mhandisi Mahundi na kuongeza:

“Tunatarajia Wanasheria mtatusaidia katika kusimamia sheria na sera mbalimbali zinazosimamia ulinzi wa taarifa,ili kuimarisha ulinzi wa hatari tunazokabiliana nazo kama vile ukiukwaji wa faragha na mashambulizi ya kimtandao,”.