December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa  

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza 

Wadau wa siasa,wametakiwa kuwaelekeza wagombea wao kutotumika lugha za matusi na kashfa katika mikutano yao ya  kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,zinazotarajiwa kuhitimishwaNovemba 26,2024.

Uchaguzi  wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika Jumatano ya Novemba 27,2024,kwa nchini nzima.

Rai hiyo imetolewa Novemba 23,2024, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa,katika mkutano wa wadau wa uchaguzi,uliofanyika uwanja wa Polisi Mabatini,jijini Mwanza,ambapo amesema katika mikutano ya kampeni,wamepanga Askari Polisi.

“Kazi yao ni kufuatilia kila neno,kama litakuwa la matusi,titawajibika kuchukua hatua za kisheria,kwani kutoa matusi unakuwa umetenda kosa la jinai,kama ni kashfa hatua za kisheria zitachukuliwa pia,”amesema Mutafungwa.

Pia ameeleza kuwa ni kosa kuondoa,kubandua au kuchana matangazo ya wagombea, wa vyama vingine,ni kosa kuandika maneno mengine katika matangazo ya wagombea wa vyama vingine vya kisiasa.

“Unakuta chama kingine kimebandika bango,na wewe unabandika juu,au unachukua maneno mengine yasiyo husiana na  bango,unabandika pale,naomba mfahamu kwamba like ni kosa na watu watakaofanya makosa kama hayo Jeshi la Polisi halitawaacha,”amesema Mutafungwa na kuongeza:

“Kazi yetu nyingine ni kuhakikisha mchakato wa kupiga kura,kuhesabu na kutangaza matokeo,mchakato wake unakuwa huru na  haki,”.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Mkoa wa Mwanza Boniphace Nkobe,amesema Mwanza hakuna mtu atakaye mwaga damu,Ina amini katika hali na amani.

“Kwa sababu tunda la amani ni haki,tumehipanga kushiriki uchaguzi,hatutajitoa,hatutakimbia uchaguzi na hatutakimbia matokeona tutatangazwa kwa mujibu wa sheria,”.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mkoa wa Mwanza (MNEC),Jamali Babu, amesema Jeshi la Polisi,lineimarika na linatimiza wajibu wake,na kutoa fursa kwa wadau wa uchaguzi  kutambua wajibu wao kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Kimsingi kuhakikisha suala la utulivu,usalama na amani,kwa wananchi wote wa Mwanza.Chama Cha Mapinduzi tumeona ni msingi ule ule kwa sababu katika ilani yetu ya chama,tukiendelea kusisitiza amani,ulinzi na utulivu kwa wananchi wote,kwani bila amani hakuna jambo litakalowezekana,”.

Babu amesema,Kamanda huyo amesisitiza zaidi kufuata sheria kwa mwananchi mmoja hata vyama vya siasa,kufuata sheria za uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Sheria zote za nchi na kanuni zake hivyo maelekezo hayo watawaelekeza wanachama wao kwani baada ya uchaguzi kuna maisha yanaendelea.